Loading...

KUMBEZA NA KUMTUPIA LAWAMA NIYONZIMA NI KUKOSA SHUKRANI

Loading...
KUMBEZA NA KUMTUPIA LAWAMA NIYONZIMA NI KUKOSA SHUKRANI - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa KUMBEZA NA KUMTUPIA LAWAMA NIYONZIMA NI KUKOSA SHUKRANI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : KUMBEZA NA KUMTUPIA LAWAMA NIYONZIMA NI KUKOSA SHUKRANI
link : KUMBEZA NA KUMTUPIA LAWAMA NIYONZIMA NI KUKOSA SHUKRANI

soma pia


KUMBEZA NA KUMTUPIA LAWAMA NIYONZIMA NI KUKOSA SHUKRANI

Mwambawahabari


19274793_451807958532321_614007456872391788_n
” shukuru kwa kila jambo Mungu ndio mpaji”
Huu ni mmoja kati ya msemo mkubwa sana katika lugha ya Kiswahili ambao huonesha au huitayarisha nafsi kuwa na mtazamo chanya kiimani.
Kinyongo ni kitu kibaya sana katika maisha ya mwanadamu . Hupofusha ufahamu na kuweka mazingira ya uovu pasipo sababu ya msingi.

Haruna Niyonzima kwa miaka kadhaa toka ajiunge na Yanga SC amesimama kama mchezaji kipenzi kwa wanayanga na hata wadau wengine wa soka nchini. Hii imetokana na kipaji chake (remarkable) uwanjani na haiba yake kiujumla.
Katika miaka sita aliyoitumikia Yanga SC ameipa mafanikio mengi akishirikiana na wenzake ; vikombe 4 vya ligi kuu 2012-13,2014-15,2015-16 na 2016-17.
Msimu wa 2013 aliibuka mchezaji bora wa ligi kuu Tanzania bara ndio msimu ambao jina la Fabregas liliposhika hatamu. Ubora wake uwanjani uliwafanya Tanga kujizolea mashabiki kila kona ya nchi na nje ya nchi hususani nchini Rwanda anapotoka kiungo huyu.
Niyonzima pia amesimama kama sehemu ya nguzo imara kuipeleka Yanga SC hatua ya makundi kombe la Shirikisho lakini muuanganiko wake na Thabani Kamusoko kwa mechi kadhaa za klabu bingwa Afrika ukisimama kama kielelezo cha ubora wake. Mechi na Al Ahly Misri na hapa nyumbani ni moja ya mechi ambazo utatamani kila saa kuzitazama.
Vikombe vitatu vinne ngao ya jamii na kombe moja la FA (ASFC ) ni vitu ambavyo vinakupa sababu ya kuinua mikono juu na kusema asante.
Wakati Yanga SC wakicheza na FC Platinum ya Zimbabwe, mmoja wa wachezaji ambao walionja joto ya jiwe ya kiungo Thabani Scara Kamusoko ni Haruna Niyonzima. Jambo hilo lilimfanya baada ya mechi kumkimbilia kocha mkuu wa Yanga SC wakati huo Hans Van Pluijm na kumsihi kumwangalia kiungo huyo na kumsajili katika kikosi chao jambo ambalo Hans aliridhia na kumsajili. Hii inaonesha mapenzi makubwa aliyokuwa nayo mchezaji huyo kwa klabu yake.
Tunaweza kuchachua nyongo zetu leo na kuamua kumchukia Haruna kisa anaondoka Yanga kwa klabu yake kushindwa kufikia dau lake lakini kuna vitu lazima tujiulize kama binadamu katika dhana ya ustaarabu wetu . Tuna haki ya kumchukia?
Mwaka 2009 Christian Ronaldo alipohama Manchester United kwenda Real Madrid, mashabiki wengi wa Old Traford waliumia sana lakini hawakumtupia lawama na mpaka leo amebaki kama balozi wao mwema zaidi kilichotokea ni kuwavuta kuishabikia timu hiyo ya Uhispania.
Haruna ana legacy kubwa kama mchezaji wa kigeni aliyewahi kudumu kwa miaka mingi katika klabu ya Yanga tena kwa mafanikio na hiki ndio kinawatesa wana Yanga SC na mbaya zaidi kuhusishwa na kuhamia kwa mahasimu wao wakubwa Simba SC. Lakini wanajangwani wanatakiwa kuelewa hili si jambo geni katika soka na kamwe alistahili chuki zaidi ya kuinua mkono wa heri. Ni nani asiyetambua mchango na thamani ya Lunyamila Yanga? lakini alivaa jezi ya msimbazi. Kizota na mapenzi yake kwa Yanga alivaa jezi ya Simba, Mohamedi Hussein moyo wa Yanga lakini pia alivaa uzi wa wekundu hao wa Msimbazi. Nemesi mmoja wa magolikipa mahiri wa Yanga miaka ya 90, alitimkia Simba pia. Wapo wengi sana.
Wanajangwani wanatakiwa kumwambia Haruna ‘asante’ na kutizama jinsi gani ya kukiimarisha kikosi chao bila yeye ili kulinda ubingwa wao na ufahari wao katika soka la Tanzania na kujaribu mafanikio mazuri kimataifa.
Ni dhahiri hali ya kiuchumi imemuondoa klabuni na sio usaliti wa aina yoyote kama ilivyokuwa kwa watangulizi wake kama Mrisho Ngasa na wengineo ambao hata siku moja hawakuwahi kuamini Yanga inaweza kuwappteza. Mpira ni ajira na biashara yao acha watafute maisha ili tusije kuwalaumu baadae licha ya ubora wao wanakufa masikini.
Hata mwaka 1994 mchezaji kipenzi wa Yanga SC aliyedumu kwa miezi 8 tu! klabuni na kujizolea umaarufu mkubwa kwa kipaji chake , Costantine Kimanda akiwa na mwenzake Ngadou Ramadhani toka Burundi alipoamua kutumkia Uarabuni kusaka maisha bora wengi waliumia lakini mpaka leo Yanga bado imesimama imara na ikishikiria rekodi yake ya kuchukua ubingwa wa ligi kuu mara nyingi zaidi.


Hivyo makala KUMBEZA NA KUMTUPIA LAWAMA NIYONZIMA NI KUKOSA SHUKRANI

yaani makala yote KUMBEZA NA KUMTUPIA LAWAMA NIYONZIMA NI KUKOSA SHUKRANI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala KUMBEZA NA KUMTUPIA LAWAMA NIYONZIMA NI KUKOSA SHUKRANI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/06/kumbeza-na-kumtupia-lawama-niyonzima-ni.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "KUMBEZA NA KUMTUPIA LAWAMA NIYONZIMA NI KUKOSA SHUKRANI"

Post a Comment

Loading...