Loading...
title : LIFE MINISTRY YATOA MSAADA WA VIFAA TIBA HOSPITALI TEULE YA MKOA SIMIYU
link : LIFE MINISTRY YATOA MSAADA WA VIFAA TIBA HOSPITALI TEULE YA MKOA SIMIYU
LIFE MINISTRY YATOA MSAADA WA VIFAA TIBA HOSPITALI TEULE YA MKOA SIMIYU
Na Stella Kalinga, Simiyu
Shirika la Kidini la Madhebu ya Kikristo la Life Ministry limetoa vifaa tiba vyenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 40 kwa Hospitali Teule ya Mkoa wa Simiyu, Mjini Bariadi.
Akipokea vifaa hivyo Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Anthony Mtaka ameishukuru Life Ministry kwa msaada huo na kuwahakikishia kuwa vifaa hivyo vitasaidia kuboresha utoaji wa huduma za afya kwa wananchi katika hospitali hiyo.
Aidha, amesema Serikali iko tayari kushirikiana na madhehebu ya dini katika kuhakikisha kuwa afya za wananchi zinakuwa salama, hivyo akawahakikishia kuwa milango iko wazi kwa taasisi nyingine za dini zinazotaka kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuboresha huduma za afya.
Mtaka ameongeza kuwa ili Madaktari na wauguzi waweze kutekeleza majukumu yao vizuri ni lazima wawezeshwe vifaa, hivyo msaada huo utawatia moyo na kuongeza ari ya kufanya kazi.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Life Ministry hapa nchini, Dismas Shekalaghe amesema vifaa hivyo vimetolewa kama sehemu ya kuisaidia jamii ambavyo vitawawezesha madaktari na wauguzi kuwahudumia wananchi.
Shekalaghe ameongeza kuwa wao wanaamini kuwa ili mtu aweze kumtumikia Mungu ni lazima awe na afya njema, hivyo kupitia msaada huo wa vifaa wagonjwa watahudumiwa na kurudi katika hali zao kawaida na kuendelea kumtumikia Mungu na kufanya shughuli za maendeleo.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(katikati), Mganga Mfawidhi wa Hospitali Teule ya Mkoa, Dkt. Fredrick Mlekwa(kushoto) wakipokea baadhi ya vifaa vilivyotolewa Life Ministry kutoka kwa Mkurugenzi wa Shirika hilo la dini, Bw. Dismas Shekalaghe(Kulia).
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(katikati), Mganga Mfawidhi wa Hospitali Teule ya Mkoa, Dkt. Fredrick Mlekwa(kushoto) wakikabidhiwa viti vya kubebea wagonjwa na Mkurugenzi wa Life Ministry Bw. Dismas Shekalaghe (kulia). ambavyo ni miongoni mwa vifaa vilivyotolewa Shirika hilo la Kikristo kwa Hospitali Teule ya Mkoa wa Simiyu.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala LIFE MINISTRY YATOA MSAADA WA VIFAA TIBA HOSPITALI TEULE YA MKOA SIMIYU
yaani makala yote LIFE MINISTRY YATOA MSAADA WA VIFAA TIBA HOSPITALI TEULE YA MKOA SIMIYU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala LIFE MINISTRY YATOA MSAADA WA VIFAA TIBA HOSPITALI TEULE YA MKOA SIMIYU mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/06/life-ministry-yatoa-msaada-wa-vifaa.html
0 Response to "LIFE MINISTRY YATOA MSAADA WA VIFAA TIBA HOSPITALI TEULE YA MKOA SIMIYU"
Post a Comment