Loading...
title : Maadhimisho Siku ya Mtoto wa Afrika: Viongozi wa Dini Wakemea Ukatili
link : Maadhimisho Siku ya Mtoto wa Afrika: Viongozi wa Dini Wakemea Ukatili
Maadhimisho Siku ya Mtoto wa Afrika: Viongozi wa Dini Wakemea Ukatili
VIONGOZI wa Dini wamekemea vitendo vya ukatili kwa watoto na kwani vimekemewa hata katika vitabu vya dini, huku wakimtaka kila mmoja kumlinda mtoto pamoja na kueneza elimu ya malezi. Viongozi hao walioshiriki katika mkutano wa vyombo vya habari ulioandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA) kutoka Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) na Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) kwa pamoja waliungana na TAMWA kukemea vitendo vya kikatili wanaofanyiwa watoto, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika.
Akizungumza Mwakilishi kutoka Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), Sheikh Shomari Mchongoma alisema jamii kwa pamoja inapaswa kuungana na kukemea vitendo vya kikatili kwani ni kinyume cha imani zetu. Alisema jambo pekee ambalo linaweza kufanikisha mapambano hayo ni jamii kumrudia mwenyezi Mungu na kukemea vitendo viovu anavyochukizwa navyo.
“…Wakati umefika tuangalie ni namna gani kumkomboa mtoto wetu kwenye wimbi la mateso ya kikatili ambayo wamekuwa wakitendewa baadhi ya watoto wetu. Mtoto anaweza kuwa salama endapo tutaungana na kukemea vitendo hivyo bila kujali tofauti zetu,” alisema Sheikh Mchongoma.
Kwa upande wake, Mwakilishi kutoka Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), Bw. Lucas Singili alisema mtoto anaitaji malezi ya pamoja kwa ushirikiano ikiwa ni kuwaweka karibu ili waweze kukua katika malezi mema. Watoto hawapaswi kutengwa wala kufanyiwa vitendo vya kikatili zaidi ya kuwapa msaada kutoka kwa wazazi, walezi na jamii kwa ujumla ili waweze kuwa raia wema wenye maadili katika taifa la baadaye.
Mwakilishi kutoka Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), Sheikh Shomari Mchongoma (kushoto) akizungumza katika mkutano wa vyombo vya habari pamoja na viongozi wa dini kutoka BAKWATA, Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) na Mtaalamu wa Saikolojia ya Jamii, John Ambrose kukemea vitendo vya kikatili dhidi ya watoto, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika.
Hivyo makala Maadhimisho Siku ya Mtoto wa Afrika: Viongozi wa Dini Wakemea Ukatili
yaani makala yote Maadhimisho Siku ya Mtoto wa Afrika: Viongozi wa Dini Wakemea Ukatili Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Maadhimisho Siku ya Mtoto wa Afrika: Viongozi wa Dini Wakemea Ukatili mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/06/maadhimisho-siku-ya-mtoto-wa-afrika.html
0 Response to "Maadhimisho Siku ya Mtoto wa Afrika: Viongozi wa Dini Wakemea Ukatili"
Post a Comment