Loading...

Matukio : Rais Dk. Shein Awaapisha Mkuu wa JKU na Mkuu wa Chuo cha Mafunzo Zanzibar

Loading...
Matukio : Rais Dk. Shein Awaapisha Mkuu wa JKU na Mkuu wa Chuo cha Mafunzo Zanzibar - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Matukio : Rais Dk. Shein Awaapisha Mkuu wa JKU na Mkuu wa Chuo cha Mafunzo Zanzibar, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Matukio : Rais Dk. Shein Awaapisha Mkuu wa JKU na Mkuu wa Chuo cha Mafunzo Zanzibar
link : Matukio : Rais Dk. Shein Awaapisha Mkuu wa JKU na Mkuu wa Chuo cha Mafunzo Zanzibar

soma pia


Matukio : Rais Dk. Shein Awaapisha Mkuu wa JKU na Mkuu wa Chuo cha Mafunzo Zanzibar



Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akimvalisha cheo cha Kamishana Mkuu wa Chuo cha Mafunzo Zanzibar Nd,Ali Abdalla Ali katika hafla iliyofanyika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja kabla alikuwa Naibu Kamishana.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akimuapisha Nd,Ali Abdalla Ali kuwa Kamishana Mkuu wa Chuo cha Mafunzo Zanzibar katika hafla iliyofanyika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja kabla alikuwa Naibu Kamishana.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akimuapisha Kanal Ali Mtumweni Hamad kuwa Mkuu wa Kikosi cha Jeshi la Kujenga Uchumi, Zanzibar (JKU ) katika hafla iliyofanyika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Balozi Seif Ali Iddi na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe.Zubeir Ali Maulid ni miongoni mwa Viongozi waliohudhurika katika hafla ya kuwapishwa Mkuu wa JKU na Kamishana Mkuu wa Chuo cha Mafunzo,katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja.

Baadhi ya Makamanda wa Kikosi cha Jeshi la Kujenga Uchumi JKU na Chuo cha Mafunzo Zanzibar wakiwa katika hafla ya kuwapishwa wakuu wao Wapya na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) katika Ukumbi wa wa Ikulu Mjini Unguja.

Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othman Makungu (kulia) Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Mhe.Said Hassan Said na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe,Ayoub Mohamed Mahmoud, ni miongoni mwa Viongozi waliohudhurika katika hafla ya kuwapishwa Mkuu wa JKU na Kamishana Mkuu wa Chuo cha Mafunzo,katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Mhe,Haji Omar Kheri (kushoto) Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi na Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji, ni miongoni mwa Viongozi waliohudhurika katika hafla ya kuwapishwa Mkuu wa JKU na Kamishana Mkuu wa Chuo cha Mafunzo,katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi mbali mbali wa Serikali baada ya kuwaapisha rasmi Kamishana Mkuu wa Chuo cha Mafunzo Zanzibar Ali Abdalla Ali kuwa (wa nne kushoto) na Kanal Ali Mtumweni Hamad Mkuu wa Kikosi cha Jeshi la Kujenga Uchumi, Zanzibar JKU (wa nne kulia) hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja. (Picha na Ikulu)




RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein leo amewaapisha Viongozi wa Vikosi vya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), aliowateua hivi karibuni kuwa Wakuu katika Vikosi hivyo.


Katika hafla hiyo, Dk. Shein kabla ya kumuapisha Naibu Kamishna wa Chuo cha Mafunzo Ali Abdalla Ali, alimfisha cheo cha Ukamishna na baadae kumuapisha kuwa Kamishna wa Chuo cha Mafunzo, Zanzibar.


Wakati huo huo, Dk. Shein, amemuapisha Kanal Ali Mtumweni Hamad kuwa Mkuu wa Kikosi cha Jeshi la Kujenga Uchumi, Zanzibar (JKU).


Hafla hiyo, ilifanyika Ikulu mjini Zanzibar na kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali akiwemo Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Idd, Spika wa Baraza la Wawakilishi Zubeir Ali Maulid, Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Said Hassan Said,


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za (SMZ), Haji Omar Kheir, Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Dk. Abdulhamid Yahya Mzee, Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabih, Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji.


Wengine ni Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohamed Mahmoud, Wakuu wa Vikosi vya SMZ, Meya wa Manispaa ya Mji wa Zanzibar Khatib Abrahman Khatib, Washauri wa Rais wa Zanzibar pamoja na viongozi wengine wa Serikali.


Hivyo makala Matukio : Rais Dk. Shein Awaapisha Mkuu wa JKU na Mkuu wa Chuo cha Mafunzo Zanzibar

yaani makala yote Matukio : Rais Dk. Shein Awaapisha Mkuu wa JKU na Mkuu wa Chuo cha Mafunzo Zanzibar Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Matukio : Rais Dk. Shein Awaapisha Mkuu wa JKU na Mkuu wa Chuo cha Mafunzo Zanzibar mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/06/matukio-rais-dk-shein-awaapisha-mkuu-wa.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Matukio : Rais Dk. Shein Awaapisha Mkuu wa JKU na Mkuu wa Chuo cha Mafunzo Zanzibar"

Post a Comment

Loading...