Loading...

MAWAKILI WATAKIWA KUJIKITA VIJIJINI

Loading...
MAWAKILI WATAKIWA KUJIKITA VIJIJINI - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MAWAKILI WATAKIWA KUJIKITA VIJIJINI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MAWAKILI WATAKIWA KUJIKITA VIJIJINI
link : MAWAKILI WATAKIWA KUJIKITA VIJIJINI

soma pia


MAWAKILI WATAKIWA KUJIKITA VIJIJINI


Mwambawahabari
Displaying Pix 00.jpg Mgeni Rasmi Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Hamis Juma (katikati) akifuatilia jambo wakati wa sherehe za 56 za kuwakubali na kuwasajiri, Mawakili wapya 248 mapema hii leo katika viwanja vya Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam.
Displaying Pix 01.jpg
Baadhi ya ndugu wa Mawakili wapya wakisubiri  zoezi la kuapishwa kwa ndugu zao mapema hii leo katika viwanja vya Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam.
Displaying Pix 02.jpg
Baadhi ya Mawakili wapya wakisubiri zoezi la kuapishwa mapema hii leo katika viwanja vya Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam.
Displaying Pix 03.jpg
Mgeni Rasmi Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Hamis Juma (wanne toka kushoto waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Majaji na Mawakili wapya mara baada ya kuwaapisha mapema hii leo katika viwanja vya Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam.Picha na Eliphace Marwa -Maelezo



Na. Eliphace Marwa – Maelezo

Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Hamis Juma amewataka Mawakili wapya kufanya kazi kwa kuzingatia maadili ya taaluma ya uwakili na kutumia taaluma zao kwa kutoa msaada wa kisheria kwa jamii. 
Aliyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam wakati wa Sherehe za 56 ya kuwapokea na kuwaapisha Mawakili wapya 248 iliyofanyika katika viwanja vya Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam.
Aidha Kaimu Jaji Mkuu amewahimiza Mawakili wapya kujiendeleza kitaaluma kwa sababu kuwa wakili sio mwisho wa taaluma kwani wanahitajika kusoma sheria za nchi mbalimbali Duniani ili kuweza kuingia mikataba ya kimataifa. 
Alisema mawakili wapya wanatakiwa washiriki katika kutoa haki, wawe waaminifu kwa mahakama na wateja kwani wakienda kinyume haki itapotea.
“Mawakili wote wanatakiwa kuwa waaminifu kwa wateja wanaowahudumia na kushirikiana na mahakama katika kutoa haki na wasiwe mawakala wa rushwa bali wawe mawakala wa kutenda haki,” alisema Kaimu Jaji Mkuu Prof. Ibrahim.
Aidha Kaimu Jaji Mkuu aliwataka mawakili hao kufika maeneo ya nje ya mji ili wasaidie upatikanaji wa haki kwani kumekuwa na changamoto kubwa ya mawakili katika maeneo ya nje ya miji.
Naye Rais wa Chama cha Wanasheria cha Tanganyika (TLS) Tundu Lissu amewataka Mawakili hao kutumia taaluma hiyo katika kuisaidia jamii kujua haki zao na utawala wa sheria japo kuna changamoto mbalimbali zinazoikabili tasnia ya sheria nchini.
“Napenda kuwatakia kila la kheri mawakili hawa wapya ila niwaombe watumie taaluma hii kwa kuisaidia jamii kujua haki zao pamoja na utawala wa sheria,” alisema Mh. Tundu Lissu.

Idadi ya mawakili walioapishwa leo imepelekea Tanzania kuwa na idadi ya zaidi ya mawakili 6300.


Hivyo makala MAWAKILI WATAKIWA KUJIKITA VIJIJINI

yaani makala yote MAWAKILI WATAKIWA KUJIKITA VIJIJINI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MAWAKILI WATAKIWA KUJIKITA VIJIJINI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/06/mawakili-watakiwa-kujikita-vijijini.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "MAWAKILI WATAKIWA KUJIKITA VIJIJINI"

Post a Comment

Loading...