Loading...

MBUNGE MLATA AHAMASISHA MICHEZO MASHULENI

Loading...
MBUNGE MLATA AHAMASISHA MICHEZO MASHULENI - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MBUNGE MLATA AHAMASISHA MICHEZO MASHULENI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MBUNGE MLATA AHAMASISHA MICHEZO MASHULENI
link : MBUNGE MLATA AHAMASISHA MICHEZO MASHULENI

soma pia


MBUNGE MLATA AHAMASISHA MICHEZO MASHULENI

MBUNGE wa viti maalumu Mkoa wa Singida,Marther Mlata amesema ili kukabiliana na utoro mashuleni pamoja na kusuasua kwa elimu,walimu hawana budi kutafuta namna ya kuwavutia watoto kupenda shule kupitia njia ya michezo.

Mbunge Mlata alitoa ushawishi huo alipokuwa akiongea na wanafunzi,wazazi na walezi wa watoto wa shule ya sekondari ya Mtakatifu Vincent iliyopo katika Mji mdogo wa Mitundu,wilayani Manyoni,Mkoani Singida.

 “Ni lazima walimu mtafute namna ya kuwavutia watoto kupenda shule,kwa mfano michezo mtu mwingine anaweza akaenda shule kwa ajili ya michezo tu anasema shuleni huwa kuna mpira,huwa wanacheza ngoja niende”alifafanua Mlata ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida.

Kwa mujibu wa Mlata mwanafunzi pindi anapokwenda shuleni kwa lengo la kushiriki katika michezo,inakuwa ni rahisi pia kumpata kwenye masomo darasani.

Aidha Mbunge huyo aliweka bayana kwamba ili kuhakikisha michezo mashuleni inawezekana kuwepo kwa kipindi chote,alitumia hafla hiyo kukabidhi mipira kumi na jezi pea kumi kwa ajili ya kugawa katika shule zilizopo katika kata ya Mitundu.

“Mimi sikuwa najua kwamba mmeongoza mmewafunga wanyiramba sisi wakimbu tumewafunga wale wanyiramba goli 3- 0 kwa hiyo nakuja kuhimiza michezo mashuleni”alibainisha Mbunge huyo mpenda michezo.

Hata hivyo aliweka bayana kwamba ndiyo maana utoro mashuleni na kusuasua kwa elimu kunakochangiwa na wanafunzi kutembea umbali mrefu kufuata masomo alilazimika kumuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Itigi kuhakikisha anazisajili shule ambazo bado hazijasajiliwa ili kuwapunguzia watoto adha ya kutembea umbali huo mrefu.

Ni Baadhi ya vifaa vya michezo vilivyotolewa msaada na Mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Singida,Marther Mlata kwa ajili ya kuhamasisha michezo katika shule zilizopo katika kata ya Mitundu,tarafa ya Itigi,wilayani Manyoni,Mkoani Singida wakati wa sherehe za Juma laa Taaluma lililoandaliwa na kata hiyo.(Picha Na Jumbe Ismailly)


Hivyo makala MBUNGE MLATA AHAMASISHA MICHEZO MASHULENI

yaani makala yote MBUNGE MLATA AHAMASISHA MICHEZO MASHULENI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MBUNGE MLATA AHAMASISHA MICHEZO MASHULENI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/06/mbunge-mlata-ahamasisha-michezo.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "MBUNGE MLATA AHAMASISHA MICHEZO MASHULENI"

Post a Comment

Loading...