Loading...
title : MKUU MPYA WA BRIGEDI YA ZANZIBAR BRIGEDIA JENERALI FADHIL OMAR NONDO AJITAMBULISHA KWA RAIS DK.SHEIN
link : MKUU MPYA WA BRIGEDI YA ZANZIBAR BRIGEDIA JENERALI FADHIL OMAR NONDO AJITAMBULISHA KWA RAIS DK.SHEIN
MKUU MPYA WA BRIGEDI YA ZANZIBAR BRIGEDIA JENERALI FADHIL OMAR NONDO AJITAMBULISHA KWA RAIS DK.SHEIN
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amekutana na Brigedia Jenerali Fadhil Omar Nondo aliyefika Ikulu mjini Zanzibar kwa ajili ya kujitambulisha baada ya kuteuliwa kuwa Mkuu mpya wa Brigedi ya Nyuki Zanzibar.
Dk. Shein alitumia fursa hiyo kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli ambaye pia, ni Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi kwa kumteua Brigedia Jenerali Fadhil Omar Nondo kushika wadhifa na kumpongeza Brigedia huyo huku akimuhakikishi kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya uongozi wake itampa mashirikiano makubwa kama ilivyofanya kwa viongozi waliokuwepo kabla yake.
Nae, Brigedia Jenerali Nondo alimuahidi Dk. Shein kuwa ataendeleza uhusiano na ushirikiano mwema ulipo kati ya Majeshi ya Ulinzi Tanznia pamoja na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar huku akisifu mashirikiano mazuri anayoyapata kutoka kwa viongozi wa Serikali na viongozi wa vikosi vya ulinzi vya SMZ na kuahidi kutoa ushirikiano kwao pamoja na kwa wananchi wote wa Zanzibar.
Brigedia Jenerali Fadhil Omar Nondo anashika nafasi ya Marehemu Bregedia Jenerali Cyril Ivor Mhaiki, aliyekuwa Kamanda wa Brigedia ya Nyuki Zanzibar, ambaye alifariki dunia tarehe 13, Disemba mwaka 2016 huko katika Hospitali ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania, Lugalo jijini Dar-es-Salaam na kuzikwa Mkoani kwao Ruvuma.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Brigedia Jenerali Fadhil Omar Nondo alipofika kujitambulisha leo Ikulu Mjini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiagana na Brigedia Jenerali Fadhil Omar Nondo baada ya mazungumzo alipofika kujitambulisha leo Ikulu Mjini Zanzibar
(Picha na Ikulu)
Hivyo makala MKUU MPYA WA BRIGEDI YA ZANZIBAR BRIGEDIA JENERALI FADHIL OMAR NONDO AJITAMBULISHA KWA RAIS DK.SHEIN
yaani makala yote MKUU MPYA WA BRIGEDI YA ZANZIBAR BRIGEDIA JENERALI FADHIL OMAR NONDO AJITAMBULISHA KWA RAIS DK.SHEIN Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MKUU MPYA WA BRIGEDI YA ZANZIBAR BRIGEDIA JENERALI FADHIL OMAR NONDO AJITAMBULISHA KWA RAIS DK.SHEIN mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/06/mkuu-mpya-wa-brigedi-ya-zanzibar.html
0 Response to "MKUU MPYA WA BRIGEDI YA ZANZIBAR BRIGEDIA JENERALI FADHIL OMAR NONDO AJITAMBULISHA KWA RAIS DK.SHEIN"
Post a Comment