Loading...

NGOMA AWATOA HOFU MASHABIKI WA YANGA SC

Loading...
NGOMA AWATOA HOFU MASHABIKI WA YANGA SC - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa NGOMA AWATOA HOFU MASHABIKI WA YANGA SC, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : NGOMA AWATOA HOFU MASHABIKI WA YANGA SC
link : NGOMA AWATOA HOFU MASHABIKI WA YANGA SC

soma pia


NGOMA AWATOA HOFU MASHABIKI WA YANGA SC

Mwambawahabari
donald-ngoma_y74s59dppwm11graq3x6da05x
SASA mashabiki wa Yanga wanaweza kuanza kutuliza presha, baada ya straika wao, Donald Ngoma, kudai kuwa kama mambo yakienda vizuri ataendelea kukitumikia kikosi chake hicho, kilichomuibua kutoka FC Platinum ya nchini Zimbabwe.
Ngoma amemaliza mkataba wake na Yanga ambapo mpaka sasa hawajafikia makubaliano yoyote, lakini taarifa zinadai kuwa uongozi unafanya kila linalowezekana kuhakikisha wanambakisha mkali huyo wa mabao.
Licha ya kwamba Simba wanamvizia, lakini upo uwezekano mkubwa Yanga wakafanikisha mpango wake wa kumzuia asiende popote kama wakiweka mkwanja wa maana, kama mchezaji mwenyewe anavyotaka.

Rafiki wa karibu wa mchezaji huyo, alisema, straika huyo hajamalizana na timu yoyote mpaka sasa na kwamba kama Yanga wakiwahi njia itakuwa nyeupe kumbakisha.
“Ni kweli Simba wanamfukuzia sana huyu jamaa (Ngoma), lakini bado hakuna makubaliano yoyote ya mkataba, licha ya kwamba wenyewe wanataka kumsainisha miaka miwili, lakini pesa ndiyo inayoonekana kuwa kikwazo, lakini kama Yanga wakiwahi wanaweza kuharibu dili hilo.
“Unajua bado Ngoma anaipenda sana Yanga, lakini tatizo linaloonekana ni kama timu yake hiyo imeishiwa fedha, ndiyo maana mipango yao inakwama, nakwambia kama watafanya mazungumzo na yeye hata leo wanaweza kufikia makubaliano mazuri,” alisema.
Akizungumzia taarifa za mchezaji huyo kutimkia Afrika Kusini, rafiki huyo alikiri na kudai kuwa amekwenda kwa masuala yake binafsi, lakini pia anaendelea kufuatilia mipango yake ya kujiunga na Mamelod Sundowns.
“Mara kwa mara amekuwa akienda huko na hata kipindi kile alipokuwa majeruhi alikwenda, kuna masuala yake anayafuatilia na pia kama ile timu yake iliyokuwa ikimhitaji kipindi kile Mamelodi Sundowns, kama bado wanayo nia ya kumchukua atafanya hivyo, lakini nikuhakikishie Yanga wakikaza buti watambakisha,” alisema.
Ngoma ni moja ya wachezaji muhimu wa Yanga ambao mikataba yao imefikia tamati na anatajwa kutaka kuondoka, huku Simba pia wakihusishwa kuitaka saini yake na taarifa zinadai kuwa alishawahi kuzungumza na kigogo mmoja wa Wekundu hao wa Msimbazi, japo hawakufikia muafaka.


Hivyo makala NGOMA AWATOA HOFU MASHABIKI WA YANGA SC

yaani makala yote NGOMA AWATOA HOFU MASHABIKI WA YANGA SC Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala NGOMA AWATOA HOFU MASHABIKI WA YANGA SC mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/06/ngoma-awatoa-hofu-mashabiki-wa-yanga-sc.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "NGOMA AWATOA HOFU MASHABIKI WA YANGA SC"

Post a Comment

Loading...