Loading...
title : RC TABORA ASEMA KUWEKA MAKUNDI KATIKA MABARAZA YANARUDISHA NYUMA MAENDELEO YA WANANCHI
link : RC TABORA ASEMA KUWEKA MAKUNDI KATIKA MABARAZA YANARUDISHA NYUMA MAENDELEO YA WANANCHI
RC TABORA ASEMA KUWEKA MAKUNDI KATIKA MABARAZA YANARUDISHA NYUMA MAENDELEO YA WANANCHI
Na Tiganya Vincent, NZEGA
Madiwani katika Halmashauri za Mkoa wa Tabora wametakiwa kuepuka kujenga makundi miongoni mwao ambayo yamekuwa yakisababisha wananchi waliowachagua kuchelewa kupata maendeleo kwa sababu ya muda mwingi kushughulikia migogoro badala ya kutatua matatizo mbalimbali ya wananchi.
Hayo yalisemwa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Bw. Aggrey Mwanri wakati akifunga mafunzo ya siku nne ya Madiwani na Watendaji wa Manispaa ya Tabora yaliyofanyika wilayani Nzega kuhusu jitihada za jamii kupitia mbinu shirikishi jamii ya fursa na vikwazo kwa maendeleo (O&OD) iliyoboreshwa na usimamizi wa fedha za miradi ya maendeleo (LGDG)
Alisema makundi yatawafanya washindwe kuwajibika vizuri na kujikuta miaka mitano ya uongozi wao inakwisha bila kuwafanyia chochote wananachi zaidi ya kupigania kuondoana katika uongozi badala kukazania maslahi ya wananchi.
“Nyie ndio mliko zamu sasa mkiendekeza makundi na migogoro isiyokwisha, mtajikuta zamu zenu zinamalizika hamjawafanyia chochote wananchi waliowachagua badala yake kupambana kila mnapokutana katika vikao vyenu ….kila kikao itakuwa sisi hatumutaki fulani atuongoze au fulani fulani hatufai” alisisitiza Mkuu huyo wa Mkoa.
Bw. Mwanri aliongeza kuwa wakimruhusu Shetani wa namna hiyo apite kati yao hakuna tena kazi wala maendeleo kwa wananchi wao waliowachagua.
SOMA ZAIDI HAPA
SOMA ZAIDI HAPA
Hivyo makala RC TABORA ASEMA KUWEKA MAKUNDI KATIKA MABARAZA YANARUDISHA NYUMA MAENDELEO YA WANANCHI
yaani makala yote RC TABORA ASEMA KUWEKA MAKUNDI KATIKA MABARAZA YANARUDISHA NYUMA MAENDELEO YA WANANCHI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala RC TABORA ASEMA KUWEKA MAKUNDI KATIKA MABARAZA YANARUDISHA NYUMA MAENDELEO YA WANANCHI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/06/rc-tabora-asema-kuweka-makundi-katika.html
0 Response to "RC TABORA ASEMA KUWEKA MAKUNDI KATIKA MABARAZA YANARUDISHA NYUMA MAENDELEO YA WANANCHI"
Post a Comment