Loading...

TANZANIA NA NORWAY KUSHIRIKIANA KATIKA MASUALA YA SIASA NA DIPLOMASIA

Loading...
TANZANIA NA NORWAY KUSHIRIKIANA KATIKA MASUALA YA SIASA NA DIPLOMASIA - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa TANZANIA NA NORWAY KUSHIRIKIANA KATIKA MASUALA YA SIASA NA DIPLOMASIA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : TANZANIA NA NORWAY KUSHIRIKIANA KATIKA MASUALA YA SIASA NA DIPLOMASIA
link : TANZANIA NA NORWAY KUSHIRIKIANA KATIKA MASUALA YA SIASA NA DIPLOMASIA

soma pia


TANZANIA NA NORWAY KUSHIRIKIANA KATIKA MASUALA YA SIASA NA DIPLOMASIA

 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga ameeleza kuwa kusainiwa kwa Mkataba wa Makubaliano (MoU) kuhusu kushirikiana katika Mashauriano ya Kisiasa na Kidiplomasia kati ya Tanzania na Norway kumefungua sura mpya ya mahusiano kati ya nchi hizo mbili. 

Kauli hiyo ameitoa leo jijini Dar Es Salaam wakati anaongea na waandishi wa habari baada ya shughuli ya uwekaji saini wa makubaliano hayo aliyoifanya kwa pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway, Mhe. Borge Brende kukamilika.

Alisema kusainiwa kwa MoU hiyo kutazifanya nchi hizo kuwa na mahusiano ya karibu zaidi katika kubadilishana mawazo kuhusu masuala ya kisiasa na kidiplomasia ambayo kimsingi yalikuwepo tokea zamani lakini leo yamerasimishwa. 

Mhe. Mahiga amewambia wanahabari kuwa Tanzania na Norway zimekuwa zikishirikiana kiuchumi, kiteknolojia na kijamii kwa takribani miaka 55 sasa. Baadhi ya maeneo aliyoyataja ambayo nchi hizo zimekuwa zikishirikiana katika kipindi hicho ni pamoja na uzalishaji wa nishati ya umeme hususan vijijini, afya, elimu, kilimo na utunzaji wa misitu. 

Mhe. Mahiga aliendelea kueleza kuwa katika kikao chao, wamejadili maeneo mapya ya ushirikiano yakiwemo utunzaji wa mazingira na kusisitiza umuhimu wa kuimarisha uhusiano wa sekta binafsi za nchi hizo mbili kinyume na awali mahusiano zaidi yalikuwa baina ya Serikali mbili.

Waziri Mahiga ameishukuru Norway kwa jitihada zake ziliozasaidia uvumbuzi na uchimbaji wa gesi asilia nchini kupitia kampuni ya Statoil ambayo imewekeza nchini mtaji mkubwa kuliko mahali popote Afrika.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (kulia) na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufalme wa Norway, Mhe. Borge Brende wakiweka saini Mkataba wa Makubaliano kuhusu kushirikiana katika Mashauriano ya Kisiasa na Kidiplomasia kati ya Tanzania na Norway.Ttukio hilo lilifanyika jijini Dar Es Salaam kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Julius Nyerere na kuhudhuriwa na Balozi wa Tanzania nchini Norway mwenye makazi yake nchini Sweden, Mhe. Dora Msechu, Balozi wa Norway nchini Tanzania, Mhe. Hanne Marie Kaarstad, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Amerika na Ulaya, Bi. Mary Matari, pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Mindi Kasiga (hawapo pichani). 
Waheshimiwa Mawaziri wakibadilishana mikataba mara baada ya kuweka saini.



Hivyo makala TANZANIA NA NORWAY KUSHIRIKIANA KATIKA MASUALA YA SIASA NA DIPLOMASIA

yaani makala yote TANZANIA NA NORWAY KUSHIRIKIANA KATIKA MASUALA YA SIASA NA DIPLOMASIA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala TANZANIA NA NORWAY KUSHIRIKIANA KATIKA MASUALA YA SIASA NA DIPLOMASIA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/06/tanzania-na-norway-kushirikiana-katika.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "TANZANIA NA NORWAY KUSHIRIKIANA KATIKA MASUALA YA SIASA NA DIPLOMASIA"

Post a Comment

Loading...