Loading...
title : Tumieni teknolojia ya Mawasiliano—Mtaalamu
link : Tumieni teknolojia ya Mawasiliano—Mtaalamu
Tumieni teknolojia ya Mawasiliano—Mtaalamu
Mary Mtuka
Teknolojia |
VIJANA wametakiwa kutumia teknolojia ya mawasiliano katika kupata fursa mbalimbali, ikiwemo sera zinazoendesha nchi na hatimaye kujikwamua kimaisha.
Mwito huo umetolewa na Mgunduzi wa Mtandao wa Platform for Policy Engagement (PUPE), Farhan Yusuf katika semina ya kuwajengea uwezo vijana na kusikiliza matatizo yao mwisho mwa wiki Dar es Salam.
Alisema mitandao hiyo ikitumika ipasavyo kwa vijana ni wazi kuwa watakuwa na uwelewa mzuri na hatimae kujikwamua kiuchumi.
Yusuf alisema kutokana na changamoto kubwa ya uwelewa mdogo wa matumizi ya mitandao ameamua kuazisha PUPE ili kusainia vijana.
"Lengo langu kubwa la kuazisha mtandao huo ni kuwasaidia vijana kupata fursa ya kujifunza sera na Sheria na mambo mbalimbali yatakayo tumika katika kuiendesha nchi," alisema.
Aliongeza kuwa asilimia kubwa ya vijana wanaokaa vijiweni wamekuwa wakilalamika huku wakiwa hawajui sera wala miongozo ambayo inahusu mitandao.
Mkurugenzi Mwenza wa Taasisi ya Sahara Sparks, inayojihusisha na kuwajengea uwezo vijana katika miradi mbalimbali ya kiteknolojia, Muda Kamata alisema wamejipanga kuwawezesha vijana hao kuazisha mitandao mingi zaidi.
Alisema pamoja na changamoto zinazowakabili vijana wemeona upo umuhimu wa kutumia njia ya mitandao ili kuweza kujua michanganuo mbalimbali ya kijamii kutokana na kuendelea kukuza kwa teknolojia.
Kwa upande wake Msimamizi wa Mawasiliano kutoka Kampuni ya Teknolojia ya CIPESA, ya nchini Uganda Bassil Malaki alitumia fursa hiyo kuwa sisitiza viongozi kutumia mitandao, kwani itasaidia kutatua kero za wananchi kwa wakati.
Hivyo makala Tumieni teknolojia ya Mawasiliano—Mtaalamu
yaani makala yote Tumieni teknolojia ya Mawasiliano—Mtaalamu Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Tumieni teknolojia ya Mawasiliano—Mtaalamu mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/06/tumieni-teknolojia-ya.html
0 Response to "Tumieni teknolojia ya Mawasiliano—Mtaalamu"
Post a Comment