Loading...
title : Umisseta Zanzibar wamerejea na vikombe vinne
link : Umisseta Zanzibar wamerejea na vikombe vinne
Umisseta Zanzibar wamerejea na vikombe vinne
Na: Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.
Zaidi ya Wanamichezo 134 kutoka Unguja na Pemba wamerejea Visiwani Zanzibar mchana wa leo Jumamosi June 17, 2017 wakitokea Butimba Mkoani Mwanza, kushiriki mashindano ya umoja wa Michezo na Sanaa skuli za sekondari Tanzania (UMISSETA).
Akizungumza na Wanamichezo hao Bandarini Malindi Mjini Unguja Naibu waziri wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Mmanga Mjengo Mjawiri amewapongeza kwa kushindana katika mashindano hayo baada ya kurejea na vikombe 4, moja cha mshindi wa kwanza na vitatu vya mshindi wa tatu.
“Kwa niaba ya Wizara ya Elimu Zanzibar nakupongezeni sana kwa ushiriki wenu wa michezo kule Mwanza, na pia nakupeni hongereni kwa kuwa na nidhamu ya hali ya juu, sisi Wizara tutaendelea na kuvitunza vipaji Mashuleni”. Alisema Mjawiri.
Mashindano hayo yaliyoanza June 6 na kumalizika juzi June 15, 2017 katika Viwanja vya Chuo cha Ualimu Butimba Mkoani Mwanza ambapo Zanzibar walifanikiwa kushinda nafasi ya kwanza kwa Wanaume kwenye mbio za Relay Mita 100 x 4, wakati kwa Mpira wa Kikapu, Wavu na mpira wa Mikono yote wakishika nafasi ya 3.
Hivyo makala Umisseta Zanzibar wamerejea na vikombe vinne
yaani makala yote Umisseta Zanzibar wamerejea na vikombe vinne Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Umisseta Zanzibar wamerejea na vikombe vinne mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/06/umisseta-zanzibar-wamerejea-na-vikombe.html
0 Response to "Umisseta Zanzibar wamerejea na vikombe vinne"
Post a Comment