Loading...
title : Unguja Kucheza Tena leo Mchezo leo Mchana Jua Kali, Bado Wanaongoza Kundi C Ambalo Lina Timu 7.
link : Unguja Kucheza Tena leo Mchezo leo Mchana Jua Kali, Bado Wanaongoza Kundi C Ambalo Lina Timu 7.
Unguja Kucheza Tena leo Mchezo leo Mchana Jua Kali, Bado Wanaongoza Kundi C Ambalo Lina Timu 7.
Wakiwa bado Vinara wa kundi “C” timu ya Unguja yenye alama 6 , kundi ambalo lina jumla ya timu 7 ambapo wapo pamoja na Katavi, Kagera, Mara, Mbeya, Iringa na Dar es salam kwenye Mashindano ya Michezo na Sanaa ya Skuli za Sekondari Tanzania (UMISSETA), mashindano ambayo yanaendelea katika viwanja vya Chuo cha Ualimu Butimba mkoani Mwanza.
Mchezo mwengine Unguja watacheza dhidi ya Mara kesho Siku ya Jumamosi ya June 10, 2017 majira ya saa 6:30 za mchana kisha michezo mengine Unguja kucheza tena Jumapili June 11, 2017 dhidi ya Mbeya, Jumatatu June 12, 2017 Unguja dhidi ya Iringa, Jumanne June 13, 2017 Unguja watamalizana na Dar es salam.
Michezo miwili ya awali Unguja juzi waliifunga Katavi 4-0, na jana wakaichapa Kagera 3-0.
KIKOSI CHA UNGUJA KILICHOPO MWANZA KATIKA MASHINDANO YA UMISSETA
WALINDA MLANGO
Aley Ali Suleiman (Ubago) na Ali Makame (Muembe ladu)
WALINZI
Ibrahim Abdallah Hamad (Arahman), Abdurahman Seif Bausi (Glorious), Abubakar Khamis (Bububu), Abdul aziz Ameir Khatib (Arahman), Ali Issa Omar (Lumumba), Ahmed Mohd Shaaban (Nyuki) na Abbas Yahya.
VIUNGO
Amani Ali Suleiman (Kiembe Samaki), Ibrahim Faraj “Mess” (Lumumba), Haji Suleiman (JKU Mtoni), Yakoub Kiparo (Langoni), Jamali Ali Jaku “Ozil” (Kinuni) na Eliyasa Suleiman (K-pura).
WASHAMBULIAJI
Faki Kombo (JKU Mtoni), Mundhir Abdallah (JKU Mtoni), Ali Hassan (Bububu), Walid Abdi “Pato” (Mwera), Ali Mohd Seif (Tumekuja) na Ali Omar (Mwera).
Hivyo makala Unguja Kucheza Tena leo Mchezo leo Mchana Jua Kali, Bado Wanaongoza Kundi C Ambalo Lina Timu 7.
yaani makala yote Unguja Kucheza Tena leo Mchezo leo Mchana Jua Kali, Bado Wanaongoza Kundi C Ambalo Lina Timu 7. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Unguja Kucheza Tena leo Mchezo leo Mchana Jua Kali, Bado Wanaongoza Kundi C Ambalo Lina Timu 7. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/06/unguja-kucheza-tena-leo-mchezo-leo.html
0 Response to "Unguja Kucheza Tena leo Mchezo leo Mchana Jua Kali, Bado Wanaongoza Kundi C Ambalo Lina Timu 7."
Post a Comment