Loading...

Wadaiwa Kodi ya Majengo kuburuzwa Mahakamani

Loading...
Wadaiwa Kodi ya Majengo kuburuzwa Mahakamani - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Wadaiwa Kodi ya Majengo kuburuzwa Mahakamani, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Wadaiwa Kodi ya Majengo kuburuzwa Mahakamani
link : Wadaiwa Kodi ya Majengo kuburuzwa Mahakamani

soma pia


Wadaiwa Kodi ya Majengo kuburuzwa Mahakamani

Nteghenjwa Hosseah, Arusha.

Wadaiwa sugu wa Kodi ya Majengo katika Jiji la Arusha watafikishwa Mahakamani mwanzoni mwa mwezi Julai endapo wataendelea kukaidi kutolipa Kodi hiyo katika kipindi hiki cha mwisho wa mwaka wa Fedha 2016/2017 unaomalizika Juni 30.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Mashaka Gambo katika kikao chake na waandishi wa habari kuwukumbusha wananchi kuhusu umuhimu wa kulipa kodi hiyo mapema kabla ya hatua kazi hazijachukuliwa wale ambao hawajalipa.

Alisema wamiliki wote wa majengo wanatakiwa kulipa Kodi hiyo kwa mujibu wa Sheria lakini hali hairidhishi kwani wengi wao hawajajitokeza kulipa wakati Serikali inategemea Fedha hizo kwa ajili ya Kutekeleza Miradi mbalimbali ya Maendeleo.

Aliongeza kuwa muda uliowekwa kwa ajili ya malipo hayo unaelekea ukikongoni:  Juni 30 itakua ni mwisho na baada ya hapo Sheria kali za Kisheria zitaanza kuchukuliwa kwa wote watakaobainika kuiibia Serikali kwa kutolipa mapato ya majengo wanayoyamiliki.

“Haiwezekani unamiliki nyumba halafu hutaki kuchangia kodi, ninatoa rai kwa wote kulipa kwa hiari kwa sababu baada ya hapo ni Faini ambayo ni mara tano ya kiasi kile ambacho ungetakiwa kulipa kwa sasa au kupelekwa Mahakami kwa mujibu wa Sheria.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo katika kikao kazi cha kuhamasisha ulipaji wa Kodi ya Majengo.
Meneja wa Mamlaka ya Mapato Mkoa wa Arusha Ndg. Apili Mbarouk akizungumza katika kikao na wanahabari cha kuwakumbusha wananchi kuhusu ulipaji wa Kodi ya Majengo.

Baadhi ya wataalam waliohudhuria katika Kikao cha Mkuu wa Mkoa kuhamasisha uhamasishaji wa Kodi ya Majengo.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA



Hivyo makala Wadaiwa Kodi ya Majengo kuburuzwa Mahakamani

yaani makala yote Wadaiwa Kodi ya Majengo kuburuzwa Mahakamani Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Wadaiwa Kodi ya Majengo kuburuzwa Mahakamani mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/06/wadaiwa-kodi-ya-majengo-kuburuzwa.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Wadaiwa Kodi ya Majengo kuburuzwa Mahakamani"

Post a Comment

Loading...