Loading...

Wananchi waomba kuhifadhi mazingira

Loading...
Wananchi waomba kuhifadhi mazingira - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Wananchi waomba kuhifadhi mazingira, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Wananchi waomba kuhifadhi mazingira
link : Wananchi waomba kuhifadhi mazingira

soma pia


Wananchi waomba kuhifadhi mazingira


Dalila Sharif

Wilaya ya Temeke
WAKAZI wa wilaya za Temeke na Kigamboni wameiomba Wakala wa Huduma za Misitu (TSF) kuwashirikisha kwa kuwapa elimu ya utunzaji  mazingira ili kunufaika nayo katika kulinda mazao yake, kuzuia uchomaji mkaa na ukataji miti ovyo.

Wakizungumza Dar es Salaam jana kwa nyakati tofauti, wananchi hao walieleza wanavyotambua wajibu wao katika utunzaji mazingira.

Mmoja wa wakazi hao kutoka Temeke, Mariam Swedi alisema ni wajibu wa kila mwananchi kushirikishwa katika utunzaji mazingira ya misitu kama mazao, uoto wa asili, nyuki, bustani na aina zingine.

“Hali hii imejitokeza kwa baadhi ya wakazi wa Dar es Salaam kukosa mwamko wa kushirikishwa katika utunzaji na ulinzi wa misitu yetu hivyo kusababisha wachache kunufaika nayo kwa uvunaji holela wa mazao ya misitu,” alisema Mariam.

Mkazi wa Kigamboni, Burhani Kambi alisema zipo baadhi ya sehemu wananchi hunufaika na mazao ya misitu hivyo hushirikisha wananchi ni jambo la msingi ili kuilinda na kuitunza, wavunaji haramu wasivamie na kuiba mazao na kukata kuni au kuchoma mkaa.

“Kwa nini wananchi tunaoishi mijini hatushirikishwi kulinda na kuitunza hata kunufaika nayo hali ambayo inabaki kusimamiwa na mawakala wa misitu pekee; watushirikishe nasi tunaweza kuiendeleza kama vijijini ambako wananchi wanajumuika kuitunza na kuwaingizia mapato,” alisema Kambi.

Pamela Oscar wa Kigamboni alisema ingawa wilaya hiyo imejaaliwa neema ya misitu kama wa Mwandege, wananchi wanastahili elimu ya juu ya umuhimu wa misitu na kuacha uharibifu wa ukataji miti ovyo pembezoni mwa wilaya hizo.


Hivyo makala Wananchi waomba kuhifadhi mazingira

yaani makala yote Wananchi waomba kuhifadhi mazingira Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Wananchi waomba kuhifadhi mazingira mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/06/wananchi-waomba-kuhifadhi-mazingira.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Wananchi waomba kuhifadhi mazingira"

Post a Comment

Loading...