Loading...

Wataka mbunge wao ajiuzulu

Loading...
Wataka mbunge wao ajiuzulu - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Wataka mbunge wao ajiuzulu, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Wataka mbunge wao ajiuzulu
link : Wataka mbunge wao ajiuzulu

soma pia


Wataka mbunge wao ajiuzulu


Abdallah Amiri, Igunga

Dk Dalaly Kafumu
BAADHI ya wananchi wa hapa wamemtaka Mbunge wao Dk Dalaly Kafumu ajiuzulu ubunge kwa walichodai ni kushindwa kutumia madaraka yake vizuri wakati akiwa Kamishna wa Madini.

Wakizungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti wilayani hapa, baadhi ya wananchi hao, Oscar Thomas, Godfrey Batoba, Pius Roben na Regina Jackson, walisema ni vema mbunge wao akajiuzulu kwa kuwa miongoni mwa wanaotuhumiwa kuiingizia hasara nchi kwa kuingia mikataba mibovu ya madini na kujinufaisha.

Thomas alibainisha kuwa kazi anayofanya Rais John Magufuli ya kufuatilia rasilimali za wananchi inapaswa kuungwa mkono na kila Mtanzania mwenye uchungu na nchi yake huku wakimwomba kutoonea huruma wahusika walioisababishia nchi hasara.

Mwenyekiti wa Wazee wa Wilaya, Kassim Ally akizungumza kwa niaba ya wazee wenzake, alisema walimwomba Rais Magufuli kutokatishwa tamaa na baadhi ya viongozi wasio waaminifu kwani wako nyuma yake wakimpa ushirikiano.

Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya, Costa Ollomi na wakem, Mwanamvua Killo walisema kazi anayofanya Rais Magufuli imeleta heshima ndani ya chama na Serikali na kuwataka wananchi kuendelea kuwa watulivu wakati waliohusika wakihojiwa na vyombo husika.

Kuhusu Mbunge kujiuzulu alisema Ollomi alisema hawezi kuzungumzia suala hilo kwa kuwa tayari Rais alishatoa maelekezo ya kuchukuliwa hatua kwa waliotajwa na Kamati.

Gazeti hili lilimtafuta Dk Kafumu kupitia simu yake ya kiganjani   ili kuzungumzia matakwa hayo lakini hakupokea simu licha ya kupigiwa zaidi ya mara nne.


Hivyo makala Wataka mbunge wao ajiuzulu

yaani makala yote Wataka mbunge wao ajiuzulu Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Wataka mbunge wao ajiuzulu mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/06/wataka-mbunge-wao-ajiuzulu.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Wataka mbunge wao ajiuzulu"

Post a Comment

Loading...