Loading...
title : Watoto wanakuja kuchukua mkono wa Idd au wametumwa kuomba?
link : Watoto wanakuja kuchukua mkono wa Idd au wametumwa kuomba?
Watoto wanakuja kuchukua mkono wa Idd au wametumwa kuomba?
Na Ummu Anfaal
Mkono wa Eid wapendwa ndugu zangu katika imaan.
Alhamdulillah Tumshukuru Allah Subhaanahu wata'ala atutakabalie swaumu zetu na tulipoteleza atughufirie na atujaalie Rehma za Mwezi wa Ramadhan. Na Neema kwenye Eid.
Awali maisha ya mwezi mtukufu wa Ramadhaan ni mazuri sana kwa hiyo tusiyawache uwe ndio mfumo wetu. Maaswi yalozuiliwa ndio tuwe tumeyafukia. Tuishi kama mwezi mtukufu. Na nina iman wengi wetu hatukuwa kwenye israaf kutokana na hali ya maisha. Kwa hiyo tutaweza kujimudu na mlo mmoja . Hakuna ulazima wa milo mitatu.
Inshaa Allah nimependa kuwasilisha hili nililolishuhudia muda mchache. Nimefikiwa na ugeni wa takriban watoto watano katika vigurupu tofauti.
Walibisha hodi na kusema mkono wa eid. Siwajui na hawanijui, lao ni kuja kuchukua eid.
Nilipowauliza wanatokea wapi ? Wamenijibu Kwa Alamshaa ni kipande na nilipokaa. Hawa watoto hawana kosa . Kosa lipo kwa wazazi. Sisi tulikulia huko miaka ya nyuma. Na hali ya maisha haikuwa kama sasa. Kila kitu kilikuwa tunu. Sasa vitu vimejaa kila mahala hakuna jipya. Ni kweli hali za maisha ni ngumu lakini wazazi tunapaswa kuwafundisha watoto wetu maadili mema .
Hii tabia ya kuranda na kuomba si nzuri. Eid wanatembeleana ndugu jamaa na marafiki. Ningependa wahusika hasa viongozi wetu wa dini kungetengwa gawio kwa wasiojiweza kwenda sehemu maalum kula eid na mwenye nacho au anotaka ku tabaruk awasilishe huko. Huu mfumo wa sasa wa kupita kuomba tusiukodolee macho tu na kunong'ona na kusengenya watoto .upo toka muaka michache ya nyuma lakini kila tukenda mambo yanazidi.
Namuunga mkono sheikh NYUNDO watoto wanatumwa kwenda KUOMBA. Haileti taswira nzuri . Allah atujaalie kheri . Amiin.
Hivyo makala Watoto wanakuja kuchukua mkono wa Idd au wametumwa kuomba?
yaani makala yote Watoto wanakuja kuchukua mkono wa Idd au wametumwa kuomba? Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Watoto wanakuja kuchukua mkono wa Idd au wametumwa kuomba? mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/06/watoto-wanakuja-kuchukua-mkono-wa-idd.html
0 Response to "Watoto wanakuja kuchukua mkono wa Idd au wametumwa kuomba?"
Post a Comment