Loading...

Wazazi wachangamkia Toto Afya Kadi ya NHIF

Loading...
Wazazi wachangamkia Toto Afya Kadi ya NHIF - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Wazazi wachangamkia Toto Afya Kadi ya NHIF, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Wazazi wachangamkia Toto Afya Kadi ya NHIF
link : Wazazi wachangamkia Toto Afya Kadi ya NHIF

soma pia


Wazazi wachangamkia Toto Afya Kadi ya NHIF

Wananchi mbalimbali wakipata huduma kwenye banda la NHIF ambapo kampeni ya usajili wa Toto Afya Kadi unafanyika. 

Na Mwandishi Wetu

KAMPENI ya usajili wa watoto chini ya Umri wa miaka 18 unaofanywa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kwenye maonesho ya 41 ya Sabasaba, umekuwa kivutio kikubwa ambapo wazazi na walezi wamepongeza mpango huo.

NHIF inaendesha kampeni hiyo chini ya mpango wa Toto Afya Kadi ambapo wazazi na walezi wanawasajili watoto wao kwa gharama ya shilingi 50,400 na kupatiwa kitambulisho cha matibabu kitakachomwezesha kupata huduma hizo ndani ya nchi.
Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Ushauri wa Kiufundi Dr. Aifena Mramba akitoa maelezo kwa wananchi waliofika bandani hapo. 

Wakizungumza kwa nyakati tofauti bandani hapo, Mkazi wa Kinondoni Bw. Ally Raymond amepongeza Mfuko kwa kuja na mpango huo ambao umekuwa ni wa nafuaa kwa wazazi na walezi ambao hawakuwa na fursa ya kupata huduma hizo.

“Kwa kweli hii ni hatua kubwa lazima tuwapongeze hasa kwa kuwajali watoto hawa chini ya umri wa miaka 18 ambao hasa ndio wana uhitaji mkubwa wa matibabu hivyo name nitoe wito kwa wazazi wengine kutumia fursa hii ili kuwa na uhakika wa matibabu wa watoto wao,” alisema Bw. Raymond.

Mzazi mwingine alipongeza hatua ya NHIF ya kusajili na kutoa vitambulisho hivyo baada ya siku moja hatua ambayo imeondoa usumbufu kwa wanaohitaji kusajili watoto wao.
Usajili wa Toto Afya Kadi ukiendelea. 

Akizungumza bandani hapo Kaimu Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti, Bi. Angela Mziray alisema kuwa hii ni fursa nzuri kwa wazazi na walezi ya kupata vitambulisho vya matibabu na kuwa na uhakika wa kupata matibabu wakati wowote na kuondokana na usumbufu ambao wangeweza kuupata.

Alisema kuwa NHIF imeanzisha mpango huo kutokana na umuhimu wa kundi la watoto ambao wameonekana kuwa na uhitaji mkubwa wa kulindwa kwa kuhakikishiwa huduma za matibabu. Jumla ya watoto 150 wameshasajiliwa na kupatiwa vitambulisho vyao.

Mbali na huduma ya usajili wa watoto, Mfuko pia unatoa huduma ya elimu kwa juu ya huduma za Bima ya Afya lakini pia kushughulikia kero mbalimbali za wanachama.
Wananchi wakilipia gharama za usajili wa Toto Afya Kadi kwa Maofisa wa Benki ya NMB.



Hivyo makala Wazazi wachangamkia Toto Afya Kadi ya NHIF

yaani makala yote Wazazi wachangamkia Toto Afya Kadi ya NHIF Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Wazazi wachangamkia Toto Afya Kadi ya NHIF mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/06/wazazi-wachangamkia-toto-afya-kadi-ya.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Wazazi wachangamkia Toto Afya Kadi ya NHIF"

Post a Comment

Loading...