Loading...
title : WAZIRI MWAKYEMBE ARIDHISHWA NA MAENDELEO YA MATENGEZO YA PITCH(SEHEMU YA KUCHEZEA) KATIKA UWANJA WA TAIFA.
link : WAZIRI MWAKYEMBE ARIDHISHWA NA MAENDELEO YA MATENGEZO YA PITCH(SEHEMU YA KUCHEZEA) KATIKA UWANJA WA TAIFA.
WAZIRI MWAKYEMBE ARIDHISHWA NA MAENDELEO YA MATENGEZO YA PITCH(SEHEMU YA KUCHEZEA) KATIKA UWANJA WA TAIFA.
Na Lorietha Laurence WHUSM.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt. Harrison Mwakyembe ameridhishwa na maendeleo ya ukarabati wa eneo la kuchezea mpira (picth) la Uwanja wa Taifa wakati wa ziara yake leo Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza katika ziara hiyo ya kukagua hatua iliyofikiwa katika matengenezo ya uwanja huo Waziri Mhe.Dkt. Mwakyembe amesema kuwa amefurahishwa na hatua ya awali ya ukarabati na anatarajia mabadiliko makubwa zaidi baada ya hatua zinazofuata kukamilika .
“Nimefurahishwa na mabadiliko niliyoyaona katika hatua hii ya awali naamini ukarabati utakapokamilika milango itakuwa wazi kwa mechi za kimataifa ikiwemo mashindano ya AFCON yanayoratajiwa kufanyika nchini kwetu mwaka 2019” alisema Dkt.Mwakyembe
Aidha aliongeza kwa kusema kuwa Serikali ipo katika mkakati wa kuhakikisha viwanja vingine vikiwemo vya mikoani vinafanyiwa ukarabati ili kuboresha sekta ya michezo nchini.
Waziri Dkt. Mwakyembe ameushukuru uongozi wa SPORTPESA kwa kuonyesha ushirikiano wa karibu na Serikali katika kuhakikisha inaweka mchango wake katika michezo kwa kukarabati sehemu ya kuchezea mpira (picth) ya Uwanja wa Taifa pamoja na vifaa mbalimbali vilivyotolewa katika kuhakikisha kazi hiyo inakamilika.
Naye Mkurugenzi wa Utawala Na Utekelezaji kutoka SPORTPESA Bw.Tarimba Abbas ameeleza kuwa kampuni yao imefanya hivyo ikiwa ni njia ya kuonyesha uzalendo wa kupenda na kuthamini vya nyumbani.
“Hatua hii ni ya awali baada ya mechi ya Everton na Gorimahiya mnamo Julai 13 mwaka huu hatua itakayofuata ni ya kuondoa nyasi zote na kuotesha mpya ambazo zitachukuwa miezi mitatu kuwa sawa” alisema Bw.Tarimba.
Uwanja wa Taifa ulianza matengenezo ya eneo la kucheze (pitch) rasmi katikati wa mwezi wa sita lengo ni kuhakikisha nyasi zilizochakaa zinaondolewa na kuwekwa nyasi mpya zitazodumu zaidi ya miaka 10 .
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe(mwenye miwani) akisikiliza maelekezo kutoka kwa Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Bw. Alex Nkenyenge (wa Tatu kulia) alipotembelea uwanja wa Taifa leo Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe (wa kwanza kushoto) akimsikiliza Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo wa Wizara hiyo Bw. Alex Nkenyenge (katikati) alipokuwa akiwatambulisha vijana ambao ni Maafisa kilimo (wenye makoti) leo Jijini Dar es Salaam , mwingine ni Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji kutoka SPORTPESA Bw.Tarimba Abbas(mwenye shati jeupe).
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) akipata maelekezo kuhusu mbegu za nyasi mpya kutoka kwa Meneja wa Uwanja wa Taifa Bw. Julius Mgaya leo Jijini Dar es Salaam alipofanya ziara ya kutembelea uwanja huo.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) akionyeshwa mashine zinazotumika katika ukarabati wa picth katika uwanja wa Taifa kutoka kwa Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Bw.Alex Nkenyenge (aliyechuchumaa), katikati ni Meneja wa Uwanja wa Taifa Bw. Julius Mgaya na kushoto ni Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji kutoka SPORTPESA Bw.Tarimba Abbas leo Jijini Dar es Salaam .
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) akielezwa jambo kuhusu matumizi mashine ya kuchorea mistari kutoka kwa Meneja wa Uwanja wa Taifa Bw. Julius Mgaya(aliyeinama) na kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Bw.Alex Nkenyenge leo Jijini Dar es Salaam alipofanya ziara ya kutembelea uwanja huo. picha na Lorietha Laurence WHUSM).
Hivyo makala WAZIRI MWAKYEMBE ARIDHISHWA NA MAENDELEO YA MATENGEZO YA PITCH(SEHEMU YA KUCHEZEA) KATIKA UWANJA WA TAIFA.
yaani makala yote WAZIRI MWAKYEMBE ARIDHISHWA NA MAENDELEO YA MATENGEZO YA PITCH(SEHEMU YA KUCHEZEA) KATIKA UWANJA WA TAIFA. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI MWAKYEMBE ARIDHISHWA NA MAENDELEO YA MATENGEZO YA PITCH(SEHEMU YA KUCHEZEA) KATIKA UWANJA WA TAIFA. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/06/waziri-mwakyembe-aridhishwa-na.html
0 Response to "WAZIRI MWAKYEMBE ARIDHISHWA NA MAENDELEO YA MATENGEZO YA PITCH(SEHEMU YA KUCHEZEA) KATIKA UWANJA WA TAIFA."
Post a Comment