Loading...

Biko yashauri washindi wake wafanye vitu vya maendeleo

Loading...
Biko yashauri washindi wake wafanye vitu vya maendeleo - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Biko yashauri washindi wake wafanye vitu vya maendeleo, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Biko yashauri washindi wake wafanye vitu vya maendeleo
link : Biko yashauri washindi wake wafanye vitu vya maendeleo

soma pia


Biko yashauri washindi wake wafanye vitu vya maendeleo

WITO umetolewa kwa washindi wa bahati nasibu ya Biko wanaoendelea kupatikana kila siku wafanye vitu vya maendeleo mara baada ya kukabidhiwa zawadi zao za fedha kutoka kwenye bahati nasibu hiyo ya aina yake.
Hayo yamesemwa na Meneja Masoko wa Biko Tanzania, Goodhope Heaven, alipokuwa anamkabidhi jumla ya Sh Milioni 20 mshindi wa Jumadili (Jumapili), Fredy Nyari, akiwa ni mshindi wa droo ya 23 ya Biko.

Akizungumzia hatua ya makabidhiano ya fedha hizo, Heaven, alisema kwamba ikiwa siku zote mtu anakosa mtaji wa kuanzisha au kuendeleza biashara zake, kupata Milioni 20 kwa mara moja si jambo la mzaha.


Alisema ni wakati wao sasa washindi wote wa Biko wale wanaopata zawadi nono ya Sh Milioni 20 inayotoka kila Jumatano na Jumapili pamoja na zawadi za papo kwa hapo zinazoanzia Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni moja wanakuza uchumi wao.

“Kwa kuanzia Sh 1,000 tu mtu anaweza kushinda 5,000 hadi Milioni 20 kwa droo zetu kubwa, ambapo ni rai yetu kwa washindi wote kuwataka maisha yao yabadilike kwa kutumia vyema fedha zao baada ya kucheza Biko, mchezo unaochezwa kwa kufanya miamala kwenye simu za TIGO Pesa, M-Pesa na Airtel Money ambapo namba yetu ya Kampuni ni 505050 na ile ya kumbukumbu ni 2456,” Alisema Heaven.


Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven, kulia akimkabidhi kiasi cha Sh Milioni 20 mshindi wao Fredy Nyari wa Kigamboni aliyeibuka na ushindi mnono wa Sh Milioni 20 katika droo ya 23 juzi. Kushoto ni Afisa wa NMB.

Mshindi wa Sh Milioni 20 wa Biko droo ya 23, Fredy Nyari, akiwa na uso wa furaha baada ya kukabidhiwa fedha zake katika benki ya NMB, jijini Dar es Salaam.
Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven kulia akiwa na mshindi wao wa Sh Milioni 20 Fredy Nyari baada ya kumkabidhi fedha zake katika benki ya NMB, jijini Dar es Salaam leo mchana.



Hivyo makala Biko yashauri washindi wake wafanye vitu vya maendeleo

yaani makala yote Biko yashauri washindi wake wafanye vitu vya maendeleo Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Biko yashauri washindi wake wafanye vitu vya maendeleo mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/07/biko-yashauri-washindi-wake-wafanye.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Biko yashauri washindi wake wafanye vitu vya maendeleo"

Post a Comment

Loading...