Loading...

Dkt. Mwakyembe atoa shukrani kwa Watanzania

Loading...
Dkt. Mwakyembe atoa shukrani kwa Watanzania - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Dkt. Mwakyembe atoa shukrani kwa Watanzania, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Dkt. Mwakyembe atoa shukrani kwa Watanzania
link : Dkt. Mwakyembe atoa shukrani kwa Watanzania

soma pia


Dkt. Mwakyembe atoa shukrani kwa Watanzania

Waziri wa Habari, Utamaduni, Michezo, Sanaa na Burudani, Dkt. Harrison Mwakyembe amewashukuru Watanzania kwa ushirikiano mkubwa waliompa katika kuombeleza kifo cha mkewe Linah Mwakyembe kilichotokea usiku wa Julai 15 mwaka huu kwenye Hospitali ya Aga Khan ya Jijini Dar es salaam.
Dkt. Mwakyembe pia amemshukuru Rais John Magufuli, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwa mchango mkubwa walioutoa katika kumuuguza mkewe.
Dkt. Mwakyembe ametoa shukrani hizo  Julai 26 wakati akizungumza na wanahabari nyumbani kwake Kunduchi wilayani Kinondoni.
Mbali na hao, Dkt. Mwakyembe ambaye pia ni Mbunge wa Kyela Mkoani Mbeya, amewashukuru viongozi wote wa dini akiwamo Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Aboubakar Zuberi na maaskofu.
"Wanafamilia tutakumbuka moyo adhimu na upendo na ushirikiano tulioupata kutoka Katibu Mkuu wa wizara hii Profesa Elisante Ole Gabriel na viongozi wengine waandamizi wa Serikali. Mwisho kabisa Wanakyela kwa uvumilivu wao katika kipindi hiki kigumu," amesema Dkt. Mwakyembe.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza na waandishi wa habari (hawapo katika picha) leo Jijini Dar es Salaam alipokuwa akitoa neno la shukrani kwa wote walioshiriki katika kumfariji kipindi cha msiba wa mke wake mpendwa Bi. Linah George Mwakyembe.


Hivyo makala Dkt. Mwakyembe atoa shukrani kwa Watanzania

yaani makala yote Dkt. Mwakyembe atoa shukrani kwa Watanzania Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Dkt. Mwakyembe atoa shukrani kwa Watanzania mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/07/dkt-mwakyembe-atoa-shukrani-kwa.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Dkt. Mwakyembe atoa shukrani kwa Watanzania"

Post a Comment

Loading...