Loading...

KAIMU JAJI MKUU ASEMA MAHAKAMA YA TANZANIA KUANZA KUSIKILIZA KESI ZA KIBENKI.

Loading...
KAIMU JAJI MKUU ASEMA MAHAKAMA YA TANZANIA KUANZA KUSIKILIZA KESI ZA KIBENKI. - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa KAIMU JAJI MKUU ASEMA MAHAKAMA YA TANZANIA KUANZA KUSIKILIZA KESI ZA KIBENKI., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : KAIMU JAJI MKUU ASEMA MAHAKAMA YA TANZANIA KUANZA KUSIKILIZA KESI ZA KIBENKI.
link : KAIMU JAJI MKUU ASEMA MAHAKAMA YA TANZANIA KUANZA KUSIKILIZA KESI ZA KIBENKI.

soma pia


KAIMU JAJI MKUU ASEMA MAHAKAMA YA TANZANIA KUANZA KUSIKILIZA KESI ZA KIBENKI.

unnamed
Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akisaini kitabu cha wageni katika katika banda la Mahakama sehemu ya Mahakama Kuu ya Tanzania. Aliyesimama mwenye miwani ni Jaji wa Mahakama Kuu 
Mhe. Edson  Mkasimongwa.

………………….
Na Magreth  Kinabo – Mahakama ya Tanzania.
5/07/2017
Kaimu   Jaji  Mkuu  wa Tanzania, Mhe. Profesa Ibrahim  Hamis  Juma, amesema  kwamba  Mahakama  ya Tanzania imejipanga  kusikiliza  kesi zilizokwama   zinazohusu   mabenki  kwamba ili ziweze kwenda kwa haraka  na  kulingana  na sera ya, ikiwemo  kuwezesha  ukuzaji wa uchumi wa  nchi .
Kauli  hiyo ilitolewa  na jana Kaimu Jaji Mkuu huyo , wakati  alipotembelea  Maonesho ya  41 ya Biashara  ya Kimataifa ya  sabasaba  yanayoendelea  katika   Viwanja  vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere vilivyoko, Barabara ya Kilwa Road jijini Dar es Salaam, ambapo  alizungumzia kuhusu mlundikano  wa kesi mahakamani  alisema Mahakama ya Tanzania  inafanya mikakati ya kuweza kuzipunguza.
“ Tunahitaji  majaji zaidi ya 30 ili kuweza kupunguza mlundikano uliopo wa kesi zilizopo Mahakamani,” alisema Profesa .
Profesa  Juma  alisema  hayo, baada ya kutembelea  mabanda  mbalimbali  ya maonesho, ambapo  alisema  Mahakama ya Tanzania,  imepiga hatua  katika mabadiliko ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano(TEHAMA), akitolea  mfano  Mahakama Kuu  ya Tanzania  Divisheni  ya Biashara, ambapo alishauri kwamba  mahakama zingine za chini ziweze kujifunza.
Profesa Juma  pia  alitoa ushauri kwa  watu wenye viwanda  nchini  kufuata  sheria  na taratibu, waweze kusajiliwa  kwa kuwa kufanya hivyo kutawafanya  washiriki kuongeza pato la Taifa na kukuza uchumi wa nchi .
“ Nimetembelea  Banda la Mkemia  Mkuu wa Serikali  nimeona  mazao na bidhaa mbalimbali,hivyo  ni vema  watu wanaotengeneza bidhaa wakasajiliwa  ili waweze kufuata  sheria  na taratibu  za nchi, kwa kuwa kufanya hivyo kutawezesha bidhaa zao kuwa bora  na  wataweza kuiwezesha nchi kushiriki katika  uchumi wa kisasa,” alisema Profesa  Juma.
 Katika  maonesho   hayo, Kaimu Jaji Mkuu huyo,  miongoni  mwa  mabanda  aliyoyatembelea  banda  la Mahakama  ya Tanzania, Jeshi  la Magereza , Banda la Jeshi la Kujenga Taifa(JKT), Chuo Kikuu cha  Dar es Salaam(UDSM),banda la   Wakala  wa  Mkemia  Mkuu wa Serikal(GCLA)i,  banda la Mamlaka ya Vitambulisho  vya Taifa(NIDA). Banda la Wakala wa Usajili , Ufilisi  na Udhamini (RITA) Mamlaka ya Reli  Tanzania, na Mabanda la Mamlaka ya Reli Tanzania, Shirika la Utangazaji Tanzania(TBC) ,Shirika la Maendeleo ya Petrol nchini (TPDC .  



Hivyo makala KAIMU JAJI MKUU ASEMA MAHAKAMA YA TANZANIA KUANZA KUSIKILIZA KESI ZA KIBENKI.

yaani makala yote KAIMU JAJI MKUU ASEMA MAHAKAMA YA TANZANIA KUANZA KUSIKILIZA KESI ZA KIBENKI. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala KAIMU JAJI MKUU ASEMA MAHAKAMA YA TANZANIA KUANZA KUSIKILIZA KESI ZA KIBENKI. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/07/kaimu-jaji-mkuu-asema-mahakama-ya_5.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "KAIMU JAJI MKUU ASEMA MAHAKAMA YA TANZANIA KUANZA KUSIKILIZA KESI ZA KIBENKI."

Post a Comment

Loading...