Loading...
title : Kamanda Mpinga Ang’olewa Usalama Barabarani.....Apelekwa Kuwa RPC Mbeya
link : Kamanda Mpinga Ang’olewa Usalama Barabarani.....Apelekwa Kuwa RPC Mbeya
Kamanda Mpinga Ang’olewa Usalama Barabarani.....Apelekwa Kuwa RPC Mbeya
IGP Sirro, amefanya mabadiliko katika jeshi la polisi ili kuboresha utendaji wa jeshi hilo kwa kumuhamisha aliyekuwa Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Mohamed Mpinga na kuwa Kamanda wa polisi wa mkoa Mbeya
Katika taarifa iliyotolewa na jeshi la polisi inasema kuwa aliyekuwa Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya (DCP) Dhahiri Kidavashari amehamishiwa Makao Makuu ya upelelezi.
Kufuatia mabadiliko hayo nafasi aliyokuwa nayo Mohamed Mpinga imechukuliwa na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Fortunatus Musilimu.
Kwa mujibu wa Barnabas Mwakalukwa (ACP) ambaye ni msemaji wa jeshi la polisi, Makao Makuu ya Jeshi hilo amesema uhamisho huo ni wa kawaida katika kuboresha utendaji wa kazi za Polisi kwa mujibu wa kanuni, taratibu na miongozo ya Jeshi la Polisi.
IGP Saimon Sirro alishauriwa na Rais John Pombe Magufuli kufanya mabadiliko katika jeshi hilo ili kuleta ufanisi na kuboresha utendaji wa jeshi la polisi nchini, jambo ambalo tayari inaonyesha ameanza kulifanyia kazi kwa kufanya mabadiliko kama haya.
Hivyo makala Kamanda Mpinga Ang’olewa Usalama Barabarani.....Apelekwa Kuwa RPC Mbeya
yaani makala yote Kamanda Mpinga Ang’olewa Usalama Barabarani.....Apelekwa Kuwa RPC Mbeya Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Kamanda Mpinga Ang’olewa Usalama Barabarani.....Apelekwa Kuwa RPC Mbeya mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/07/kamanda-mpinga-angolewa-usalama.html
0 Response to "Kamanda Mpinga Ang’olewa Usalama Barabarani.....Apelekwa Kuwa RPC Mbeya"
Post a Comment