Loading...
title : MAHAKAMA YAMFUATA MANJI HOSPITAL, ASOMOMEWA MASHTAKA YA UHUJUMU UCHUMI
link : MAHAKAMA YAMFUATA MANJI HOSPITAL, ASOMOMEWA MASHTAKA YA UHUJUMU UCHUMI
MAHAKAMA YAMFUATA MANJI HOSPITAL, ASOMOMEWA MASHTAKA YA UHUJUMU UCHUMI
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo imelazimika kuhamishia shughuli zake katika Hospitali ya taifa ya Muhimbili kwa Muda kumsomea mfanyabiashara Yusufali Manji (41), mashitaka ya uhujumu uchumi yanayomkabili.
Manji amesomewa mashtaka hayo katika Taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete iliyopo Hospitalini hapo mbele ya Hakimu Mkazi Huduma Shaidi.
Katika kesi hiyo, Manji anashitakiwa pamoja na wenzake watatu, Meneja Rasilimali watu wa Kampuni ya Quality Group Ltd, Deogratius Kisinda (28), Mtunza stoo, Abdallah Sangey (46) na Thobias Fwere (43) mkazi wa Chanika, ambapo wote watatu wamesomewa mashtaka yao katika Mahakama hiyo kabla haijaamia Muhimbili kuanzia muda wa saa Tisa alasili na kumalizima SAA 16:41
Mahakama ilifikia uamuzi wa kuhamia Muhimbili baada ya Manji kuwa amelazwa Hospitalini hapo akisumbuliwa na ugonjwa wa moyo na kulazimika kusomewa mashtaka yake akiwa kitandani.
Akisoma mashtaka hayo, wakili Mwandamizi wa Serikali, Tulumanywa Majigo amedai, Juni 30, mwaka huu huko Chang’ombe A wilayani Temeke jijini Dar es Salaam, washitakiwa wote kwa pamoja, walikutwa na askari polisi wakiwa na mabalo 35 ya vitambaa vinavyotumika kutengenezea sare za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) vyenye thamani ya milioni 192.5.
Imedaiwa kuwa, Julai Mosi mwaka huu, maeneo hayo hayo, washitakiwa wote walikutwa na askari polisi wakiwa na mabalo nane ya vitambaa vinavyotumika kutengenezea sare za JWTZ vyenye thamani ya milioni 44.
Aidha imedaiwa kuwa, Juni 30, washitakiwa hao walikutwa wakiwa na mhuri wa JWTZ ambao uliandikwa ‘’Mkuu wa Kikosi 121 Kikosi cha JWTZ’’ bila kuwa na uhalali kitendo kinachohatarisha usalama wa nchi.
BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI
BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI
Hivyo makala MAHAKAMA YAMFUATA MANJI HOSPITAL, ASOMOMEWA MASHTAKA YA UHUJUMU UCHUMI
yaani makala yote MAHAKAMA YAMFUATA MANJI HOSPITAL, ASOMOMEWA MASHTAKA YA UHUJUMU UCHUMI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MAHAKAMA YAMFUATA MANJI HOSPITAL, ASOMOMEWA MASHTAKA YA UHUJUMU UCHUMI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/07/mahakama-yamfuata-manji-hospital.html
0 Response to "MAHAKAMA YAMFUATA MANJI HOSPITAL, ASOMOMEWA MASHTAKA YA UHUJUMU UCHUMI"
Post a Comment