Loading...

Majaliwa aipongeza NHC kujenga zahanati

Loading...
Majaliwa aipongeza NHC kujenga zahanati - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Majaliwa aipongeza NHC kujenga zahanati, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Majaliwa aipongeza NHC kujenga zahanati
link : Majaliwa aipongeza NHC kujenga zahanati

soma pia


Majaliwa aipongeza NHC kujenga zahanati


Mwandishi Wetu, Lindi 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa ameupongeza uongozi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kwa kukamilisha ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Mnolela mkoani hapa kwa muda mfupi.

Amesema ujenzi wa zahanati hiyo ya kisasa ulianza Machi na sasa umekamilika, jambo ambalo litarahisisha upatikanaji huduma za afya kwa wananchi wa eneo hilo na jirani.

Waziri Mkuu alitoa pongezi hizo juzi alipozungumza na wananchi wa kijiji cha Mnolela baada ya kuzindua zahanati hiyo iliyosimamiwa na NHC.

Alisema ujenzi wa zahanati hiyo ni mwendelezo wa mkakati wa Serikali kuboresha huduma za afya kwa kuzisogeza karibu na wananchi.

“Rais John Magufuli amedhamiria kuondolea wananchi changamoto za huduma za afya, hivyo tuendelee kumwunga mkono,” alisema Waziri Mkuu.

Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Nehemia Mchechu alisema mradi wa ujenzi wa zahanati hiyo ulisimamiwa na shirika lake kwa Sh milioni 65.5.

“Sh milioni 15 zilitolewa na Rais, Sh milioni 10 na Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye huku NHC ikitoa Sh milioni 10 na kiasi kilichosalia ni mchango wa Halmashauri,” alisema.

Awali Nape alimshukuru Rais Magufuli kwa mchango mkubwa alioutoa kwenye ujenzi wa zahanati hiyo.

Nape alisema zahanati hiyo ni mkombozi kwa wakazi wa kijiji cha Mnolela na wananchi wengine wanaoishi maeneo jirani.


Hivyo makala Majaliwa aipongeza NHC kujenga zahanati

yaani makala yote Majaliwa aipongeza NHC kujenga zahanati Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Majaliwa aipongeza NHC kujenga zahanati mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/07/majaliwa-aipongeza-nhc-kujenga-zahanati.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Majaliwa aipongeza NHC kujenga zahanati"

Post a Comment

Loading...