Loading...
title : Manispaa kuzawadia Shehiya zitakazojipanga vizuri katika uhifadhi na utunzaji mazingira
link : Manispaa kuzawadia Shehiya zitakazojipanga vizuri katika uhifadhi na utunzaji mazingira
Manispaa kuzawadia Shehiya zitakazojipanga vizuri katika uhifadhi na utunzaji mazingira
Na Maryam Kidiko – Maelezo
Baraza la Manispaa Wilaya ya Mjini linakusudia kutowa zawadi kwa shehiya za Wilaya hiyo ziakazofanya vizuri zaidi katika uhifadhi na utunzaji Mazingira.
Akizungumza na Waandishi wa Habari katika Kituo cha afya Chumbuni Mkurugenzi wa Baraza hilo Aboud Hassan Serenge alisema lengo la kutoa zawadi hizo ni kuwashajiisha wanachi kujenga tabia ya kutunza mazingira ikiwa ni moja ya njia ya kupambana na maradhi ya mripuko.
Alisema Baraza la Manispaa litaendelea kushirikiana na viongozi wa Majimbo ya Wilaya hiyo kwa kutoa Vifaa vya kufanyia usafi ili kuhakikisha Mazingira ya mji yanakuwa salama kwa maisha ya wananchi .
“Sisi kama Baraza la Manispaa nijukumu letu kuhakikisha Mazingira yanakuwa masafi hivyo tutashirikiana kwa karibu na Majimbo kutowa Vifaa vya usafi ili kuhakikisha Mji wetu unakuwa katika hali ya usalama “Alisema Mkurugenzi huyo.
Hata hivyo alisema kuwa kwa wale ambao watajikusanya pamoja na kufanya usajili unaokubalika watawatengenezea mazingira mazuri ya kuhakikisha wanapata ada ya kazi wanayoifanya sambamba na ada ya Vifaa.
Vile vile alieleza kuwa miongoni mwa vitu wanavyo zingatia katika Bajeti yao ni kutoa vifaa kwa ajili ya usafi wa mazingira ili kuepusha kutokea kwa maradhi ya Miripuko .
Sheha wa Shehia ya Kwamtumwajeni, Jimbo la Magomeni, Rajab Ali Ngauchwa alisema suala la usafi wa mazingira amelipokea vizuri na kwa kushirikiana na wananchi ameahidi watalisimamia kwa ukamilifu licha ya chaangamoto ziliopo.
Alizitaja Changamoto hizo kuwa ni pamoja na muitiko mdogo wa baadhi ya wananchi juu ya suala hilo, ukosefu wa vifaa na kukosekana Sehemu ya kuwekea taka (Madampo).
Sheha Ngauchwa amewataka Wananchi wa Shehia yake kurejesha utamaduni wa zamani wa kusafisha mazingira yaliyowazunguka kwa hiari bila ya kushurutishwa jambo ambalo litasaidia kufanikisha kuweka Mazingira Safi.
“Ningependa kuwasisitiza tushirikiane pamoja kuweza kuweka mazingira yetu kuwa safi bila ya kutegemeana na kubaguwana kwa Siasa zetu kwani suala la usafi halitaki siasa,”Alisema Ngauchwa.
Nao Wananchi kutoka Shehia mbali mbali Jimbo la Magomeni Walisema kuwa suala la kuweka Mazingira safi sio suala la kuwaachia Manispaa kufanya usafi peke yao bali suala hilo linamuhusu kila mmoja wetu.
Sambamba na hayo wamesema suala la kutunza mazingira ni suala muhimu na kila mmoja anajukumu la kuhakikisha mazingira yaliyomzunguka yanakuwa salama wakati wote.
Hivyo makala Manispaa kuzawadia Shehiya zitakazojipanga vizuri katika uhifadhi na utunzaji mazingira
yaani makala yote Manispaa kuzawadia Shehiya zitakazojipanga vizuri katika uhifadhi na utunzaji mazingira Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Manispaa kuzawadia Shehiya zitakazojipanga vizuri katika uhifadhi na utunzaji mazingira mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/07/manispaa-kuzawadia-shehiya.html
0 Response to "Manispaa kuzawadia Shehiya zitakazojipanga vizuri katika uhifadhi na utunzaji mazingira"
Post a Comment