Loading...

MASAUNI AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA PWANI, AAMURU KAMANDA WA TRAFIKI MKOANI HUMO AONDOLEWE

Loading...
MASAUNI AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA PWANI, AAMURU KAMANDA WA TRAFIKI MKOANI HUMO AONDOLEWE - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MASAUNI AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA PWANI, AAMURU KAMANDA WA TRAFIKI MKOANI HUMO AONDOLEWE, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MASAUNI AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA PWANI, AAMURU KAMANDA WA TRAFIKI MKOANI HUMO AONDOLEWE
link : MASAUNI AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA PWANI, AAMURU KAMANDA WA TRAFIKI MKOANI HUMO AONDOLEWE

soma pia


MASAUNI AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA PWANI, AAMURU KAMANDA WA TRAFIKI MKOANI HUMO AONDOLEWE

Na Felix Mwagara (MOHA)


NAIBU Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, amelitaka Jeshi la Polisi kumuondoa katika nafasi ya Mkuu wa Polisi, Usalama Barabarani (RTO) Mkoa wa Pwani na kuchukuliwa hatua za kinidhamu kutokana kwa kushindwa kusimamia sheria za usalama barabarani mkoani humo.

Masauni akiwa ameambatana na Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Fortunatus Musilimu, alitoa agizo hilo katika Kituo cha Mabasi cha mjini Kibaha Maili Moja baada ya kufanya ziara ya kushtukiza kituoni hapo leo, kwa ajili ya kufuatilia maelekezo yake aliyoyatoa alipofanya ziara kama hiyo mwaka jana.

“Mwaka jana nilipofanya ziara kituoni hapa nilitoa maelekezo nilipokuta kuna mapungufu katika ukaguzi wa magari, tukakubaliana atayafanyia kazi haraka iwezekanavyo, lakini hakuna mabadiliko yoyote, magari hayakaguliwi, huku ni kuhatarisha usalama wa abiria,” alisema Masauni na kuongeza kuwa;

“RTO ameshindwa kuendana na kasi ya awamu ya tano, nataka aondolewe katika nafasi hiyo na achukuliwe hatua ya kinidhamu, hatutati uzembe, hatutaki kucheza na maisha ya watanzania.”

Masauni mara baada ya ukaguzi wa kituo hicho, aliendelea na ziara yake mkoani Pwani ambapo alifanya ukaguzi wa aina hiyo mjini Chalinze na baadaye Msata na kuimalizia ziara yake Bagamoyo.

 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akiwauliza maswali abiria wa basi la Safari Express lifanyalo safari zake Dar es Salaam kwenda Arusha, wakati kiongozi huyo alipofanya ziara ya kushtukiza katika Kituo cha Mabasi, Kibaha Maili Moja, mkoani Pwani. Masauni aliiagiza Jeshi la Polisi kumuondoa Mkuu wa Polisi, Usalama Barabarani (RTO) Mkoa wa Pwani katika nafasi hiyo na achukuliwe hatua za kinidhamu kutokana kwa kushindwa kufanya ukaguzi wa magari na kusimamia sheria za usalama barabarani mkoani humo.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akimpa maelekezo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Kamishna Msaidizi, Jonathan Shana, wakati kiongozi huyo alipofanya ziara ya kushtukiza katika Kituo cha Mabasi Kibaha Maili Moja, mkoani Pwani. Masauni alimuagiza Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Fortunatus Musilimu (wapili kulia) kumuondoa Mkuu wa Polisi, Usalama Barabarani (RTO) Mkoa wa Pwani, Abdi Isango (wapili kushoto) katika nafasi hiyo na achukuliwe hatua za kinidhamu kutokana kwa kushindwa kukagua magari na kusimamia sheria za usalama barabarani mkoani humo.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (aliyevaa suti) akiwa katika ukaguzi wa mabasi katika kituo cha mabasi cha Kibaha Maili Moja, mkoani Pwani ambapo alifanya ziara ya kushtukiza kituoni hapo. Masauni alimuagiza Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Fortunatus Musilimu (kulia) kumuondoa Mkuu wa Polisi, Usalama Barabarani (RTO) mkoani humo katika nafasi hiyo na achukuliwe hatua za kinidhamu kutokana kwa kushindwa kufuata maelekezo aliyowahi kupewa ya kukagua magari na kusimamia sheria za usalama barabarani.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akimpa maelekezo Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Fortunatus Musilimu (kulia) wakati alipokua anazungumza na askari wa usalama barabarani katika eneo la Sanzale, Bagamoyo. Masauni alifanya ziara ya kushtukiza Kituo cha Mabasi Kibaha, Chalinze pamoja na kukagua barabara hadi kufika mjini Bagamoyo.


Hivyo makala MASAUNI AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA PWANI, AAMURU KAMANDA WA TRAFIKI MKOANI HUMO AONDOLEWE

yaani makala yote MASAUNI AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA PWANI, AAMURU KAMANDA WA TRAFIKI MKOANI HUMO AONDOLEWE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MASAUNI AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA PWANI, AAMURU KAMANDA WA TRAFIKI MKOANI HUMO AONDOLEWE mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/07/masauni-afanya-ziara-ya-kushtukiza_19.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "MASAUNI AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA PWANI, AAMURU KAMANDA WA TRAFIKI MKOANI HUMO AONDOLEWE"

Post a Comment

Loading...