Loading...
title : MAWAZIRI WATANO WA TANZANIA NA UGANDA WAFANYA ZIARA MPAKANI MWA NCHI HIZO
link : MAWAZIRI WATANO WA TANZANIA NA UGANDA WAFANYA ZIARA MPAKANI MWA NCHI HIZO
MAWAZIRI WATANO WA TANZANIA NA UGANDA WAFANYA ZIARA MPAKANI MWA NCHI HIZO
Mawaziri watano wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania watembelea mpaka wa Tanzania na Uganda ili kutatua changamoto zinazoukabili mpaka huo na kuuboresha.
Mawaziri hao ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Hamad Masauni, Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Suleman Jaffo, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Suzan Kolimba na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Mhandisi Isack Kamwelwe.
Miongoni mwa maeneo yaliyotembelewa na Mawaziri hao ni eneo la mpaka ya Tanzania na Uganda kwa upande unapo pita mto Kagera na eneo la kivuko cha mpaka wa Tanzania na Uganda kilichopo Mtukula mkoani Kagera.
Katika ziara hii Mawaziri hao wameweza kujionea hali halisi ya maisha ya wakazi wa mipakani na jinsi wanavyohusiana na wenzao wa nchi ya jirani ya Uganda ambapo wamekuwa wakishirikiana na kuishi kwa amani katika shughuli zao za kila siku.Aidha, ziara hii ni maandalizi ya Mkutano wa ujirani mwema kati ya Mawaziri wa serikali ya Uganda na Mawaziri kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambao unatarajiwa kufanyika mnamo tarehe 29 Julai 2017, Bukoba mkoani Kagera.
Hivyo makala MAWAZIRI WATANO WA TANZANIA NA UGANDA WAFANYA ZIARA MPAKANI MWA NCHI HIZO
yaani makala yote MAWAZIRI WATANO WA TANZANIA NA UGANDA WAFANYA ZIARA MPAKANI MWA NCHI HIZO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MAWAZIRI WATANO WA TANZANIA NA UGANDA WAFANYA ZIARA MPAKANI MWA NCHI HIZO mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/07/mawaziri-watano-wa-tanzania-na-uganda.html
0 Response to "MAWAZIRI WATANO WA TANZANIA NA UGANDA WAFANYA ZIARA MPAKANI MWA NCHI HIZO"
Post a Comment