Loading...
title : RC MAKONDA: NAWAPA SIKU SABA WAKUU WA SHULE ZA SEKONDARI, PAMOJA NA WALIMU WAKUU WA SHULE ZA MSINGI,MUWASILISHA CHANGAMOTO ZENU ZA KAZI
link : RC MAKONDA: NAWAPA SIKU SABA WAKUU WA SHULE ZA SEKONDARI, PAMOJA NA WALIMU WAKUU WA SHULE ZA MSINGI,MUWASILISHA CHANGAMOTO ZENU ZA KAZI
RC MAKONDA: NAWAPA SIKU SABA WAKUU WA SHULE ZA SEKONDARI, PAMOJA NA WALIMU WAKUU WA SHULE ZA MSINGI,MUWASILISHA CHANGAMOTO ZENU ZA KAZI
Rc Makonda akijadiliana jambo na Afisa Elimu wa Mkoa Dar es salaam hivi leo alipokutana na wadau wa Elimu katika kujadili changamoto mbalimbali za kielimu kwa mkoa wa Dar es salaam.
Hawa ni Baadhi ya Wadau wa Elimu katika mkoa wa dar es salaam,waliohudhuria mkutano na mkuu wa mkoa hivi leo
mwambawahabari
Mkuu wa mkoa wa dar es salaamu Rc Paul Makonda amewataka walimu wakuu wa shule za msingi, wakuu wa shule za sekondari, kuwasilisha changamoto kutoka katika shule zao kwa lengo la kuboresha elimu, katika mkoa wa dar es salaam.
Rc Makonda ameyazungumza hayo Leo katika ukumbi mikutano wa kimataifa wa mwalimu Julius Nyerere Conventional Center ambapo amekutana na maafisa elimu kata, walimu wakuu wa shule za msingi, na wakuu wa shule zasekondari na kuwapa siku saba waweze kuwasilisha changamoto mbalimbali kutoka katika shule zao na kuweza kuwasilisha kwa Afisa elimu ili ziweze kufanyiwa kazi na ufaulu wa wanafunzi katika mkoa huu waweze kufanya vizuri.
"Walimu wangu wakuu niambieni changamoto zote zinazofanya usifanye vizuri katika shule yako mkae na walimu wenu waweze kuwapa changamoto zote ili niweze kuzipatia ufumbuzi" Alisema Makonda.
Pia Rc Makonda amewahakikishia wakuu hao kuanza kwa kujenga ofisi za walimu,vyoo,pamoja na furniture , kwa shule zenye changamoto izo na kwamba haya ndio ataanza nayo akisubiri waweze kuwakilisha changamoto zao. Aidha amewapa siku ishirini wakuu wa shule kuondoa gest house pamoja na baa zilizopo ndani ya shule ambazo zina changamoto iyo.
Aidha amewataka wakuu hao kuwapa nafasi walimu wao ili kuweza kutoa changamoto zao ambapoa amesema atatembelea baadhi ya shule na kukutana na walimu ili apate kujua changamoto zao na pia Makonda amewaahidi maafisa elimu kata kuwapatia pikipiki mwezi ujao za kuweza kufanya ufuatiliaji wa maendeleo ya shule katika kata zao.
Katika hatua nyingine Rc Makonda amemwagiza Afisa elimu kuwashusha vyeo baadhi ya maafisa elimu kata ambapo walikuwa wakiomba kuongezewa posho ya kwenda kutembelea maendeleo ya shule zilizopo katika kata zao,ambapo wanalipata laki mbili na nusu kama posho ya kila mwezi ambapo wao wanazitumia kwa manufaa yao binafsi. Wakidai ni posho ya cheo.
"Afisa elimu wa mkoa uwashushe vyeo na kuwapanga katika shule zenye upungufu wa walimu,pamoja na kuwatafutia adhabu nyingine,inawezekana wametuaribia hata na fikra za walimu wengine, walimu wengine wanalalamika mishahara inaechelewa lakini wengine wanafurahia kupata posho ya cheo serikali hii ya awamu ya tano haina fedha za mchezo mchezo hata mimi mwenyewe sina posho ya cheo.Nataka wapangwe kwenye shule ambapo hazina waalimu"Alisema Makonda.
Hivyo makala RC MAKONDA: NAWAPA SIKU SABA WAKUU WA SHULE ZA SEKONDARI, PAMOJA NA WALIMU WAKUU WA SHULE ZA MSINGI,MUWASILISHA CHANGAMOTO ZENU ZA KAZI
yaani makala yote RC MAKONDA: NAWAPA SIKU SABA WAKUU WA SHULE ZA SEKONDARI, PAMOJA NA WALIMU WAKUU WA SHULE ZA MSINGI,MUWASILISHA CHANGAMOTO ZENU ZA KAZI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala RC MAKONDA: NAWAPA SIKU SABA WAKUU WA SHULE ZA SEKONDARI, PAMOJA NA WALIMU WAKUU WA SHULE ZA MSINGI,MUWASILISHA CHANGAMOTO ZENU ZA KAZI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/07/rc-makonda-nawapa-siku-saba-wakuu-wa.html
0 Response to "RC MAKONDA: NAWAPA SIKU SABA WAKUU WA SHULE ZA SEKONDARI, PAMOJA NA WALIMU WAKUU WA SHULE ZA MSINGI,MUWASILISHA CHANGAMOTO ZENU ZA KAZI"
Post a Comment