Loading...
title : RC NCHIMBI : WATUMISHI PUNGUZENI KULALAMIKA
link : RC NCHIMBI : WATUMISHI PUNGUZENI KULALAMIKA
RC NCHIMBI : WATUMISHI PUNGUZENI KULALAMIKA
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi amewataka watumishi kupunguza malalamiko na kuelekeza nguvu zao katika kuhudumia wananchi kwa mambo yanayoonekana kwa macho.
Dkt Nchimbi ameyasema hayo katika baraza maalumu la madiwani wa halmashauri ya Itigi ambapo amewataka watumishi na watendaji kupunguza muda wa vikao ili waende kuwatumikia wananchi.
Amesema kumekuwa na tabia ya kulalamika ambayo pia inaambukiza kwa watumishi na watendaji wengine badala ya kutoa suluhisho kwa changamoto ambazo zitawasaidia wananchi.
Dkt Nchimbi ameongeza kuwa watendaji na madiwani wasitumie muda mwingi ofisini pamoja na kusubiria taarifa za makaratsi ambazo hazina uhalisia wa matukio na hali halisi inayoendelea kwa wananchi.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi akimkabidhi Mwenyekiti wa halmashauri ya itigi Ally Minja cheti cha mafunzo ya usimamizi wa miradi ya serikali.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi akizungumza na watumishi, watendaji na madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Itigi (hawapo pichani).
Baadhi ya watumishi wa halmashauri ya Wilaya ya Itigi wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi.
Mkaguzi wa Nje wa Hesabu za Serikali Anna Kakunguru akizungumza katika baraza maalumu la halmashauri ya Wilaya ya Itigi.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala RC NCHIMBI : WATUMISHI PUNGUZENI KULALAMIKA
yaani makala yote RC NCHIMBI : WATUMISHI PUNGUZENI KULALAMIKA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala RC NCHIMBI : WATUMISHI PUNGUZENI KULALAMIKA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/07/rc-nchimbi-watumishi-punguzeni.html
0 Response to "RC NCHIMBI : WATUMISHI PUNGUZENI KULALAMIKA"
Post a Comment