Loading...
title : SITAVUMILIA HATI CHAFU KATIKA HALMASHAURI YOYOTE MKOANI KWANGU-DKT NCHIMBI
link : SITAVUMILIA HATI CHAFU KATIKA HALMASHAURI YOYOTE MKOANI KWANGU-DKT NCHIMBI
SITAVUMILIA HATI CHAFU KATIKA HALMASHAURI YOYOTE MKOANI KWANGU-DKT NCHIMBI
Mkuu wa Mkoa wa Singia Dkt Rehema Nchimbi amesema hatavumilia kuona halmashauri inafanya uzembe na kupata hati chafu ya Mkaguzi na Mdhibiti wa Fedha za Serikali kwakuwa itamchafua yeye na taswira ya uongozi wote wa Mkoa wa Singida.
Dkt Nchimbi ametoa kauli hiyo mapema jana wakati wa baraza maalumu la madiwani wa Manispaa ya Singida la kujadili hoja za Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za serikali ambazo amesema hoja nyingi zimetokana na uzembe.
Amesema licha ya kuipongeza Manispaa ya Singida kwa kupata hati safi, uwepo wa hoja umedhihirisha kuwa kuna baadhi ya watendaji wanafanya kazi kwa uzembe na kutofuata taratibu na sheria hivyo wajirekebishe haraka.
Dkt Nchimbi ameongeza kuwa hoja nyingi zinajitokeza kwa kukosa umakini na watendaji kufanya kazi kwa mazoea hali ambayo ikiendelea inaweza kuipelekea manispaa kupata hati isiyoridhisha hivyo kupata hati safi kuwaongezee nguzu ya kuboresha utendaji kazi wao.
Aidha amewashauri wakuu wa idara na watumishi wengine kuitendea haki manispaa yao kwa kuchapa kazi kuwa wadilifu na kufuata sheria kwani wakifanya hivyo wataepuka hoja zisizo za lazima na kuharakisha maendeleo.
Mkuu wa Mkoa wa Singia Dkt Rehema Nchimbi akizungumza na Meya wa Manispaa ya Singida Gwae Chima Mbua kabla ya kuanza kwa baraza Maalumu la madiwani wa Manispaa ya Singida kujadili hoja za Mkaguzi wa Fedha za Serikali.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida Bravo Kizito Lyampembile akifungua baraza Maalumu la madiwani wa Manispaa ya Singida kujadili hoja za Mkaguzi wa Fedha za Serikali.
Baadhi ya Viongozi wa Manispaa ya Singida wakifuatilia baraza Maalumu la madiwani wa Manispaa ya Singida kujadili hoja za Mkaguzi wa Fedha za Serikali.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala SITAVUMILIA HATI CHAFU KATIKA HALMASHAURI YOYOTE MKOANI KWANGU-DKT NCHIMBI
yaani makala yote SITAVUMILIA HATI CHAFU KATIKA HALMASHAURI YOYOTE MKOANI KWANGU-DKT NCHIMBI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala SITAVUMILIA HATI CHAFU KATIKA HALMASHAURI YOYOTE MKOANI KWANGU-DKT NCHIMBI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/07/sitavumilia-hati-chafu-katika.html
0 Response to "SITAVUMILIA HATI CHAFU KATIKA HALMASHAURI YOYOTE MKOANI KWANGU-DKT NCHIMBI"
Post a Comment