Loading...
title : Vijana washauriwa kujiunga na awamu ya tatu ya program ya Via Jiandalie Ajira
link : Vijana washauriwa kujiunga na awamu ya tatu ya program ya Via Jiandalie Ajira
Vijana washauriwa kujiunga na awamu ya tatu ya program ya Via Jiandalie Ajira
Vijana wenye umri wa miaka 18 hadi 24 wameshauriwa kujiunga na awamu ya tatu ya program Via Jiandalie Ajira inayoendeshwa na Taasisi ya Ujasiriamali na Ushindani Tanzania (TECC) ili kupata mafunzo ya ujasiriamali, stadi za maisha, malezi ya kibiashara na kuunganishwa na taasisi za kifedha kupata mitaji kukabiliana na tatizo la ajira.
Meneja Malezi wa Taasisi hiyo, Bw. Daniel Mghwira alisema hayo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari, kuwa vijana wajiunge na program hiyo ambayo imeingia katika awamu ya tatu kupata mafunzo hayo ili kukabiliana na tatizo la ajira.
“Via Jiandalie Ajira awamu ya tatu inawalenga vijana wa Halmashauri zote za Mkoa wa Dar es Salaam, Mikindani Mtwara, Dodoma na Kibaha Pwani,” na fomu za kujiunga zinapatikana katika ofisi za kata, ofisi za maafisa vijana za manispaa za maeneo hayo, aliongeza kusema Bw. Mghwira ambaye pia ni Naibu Mkurugenzi wa taasisi hiyo.
Meneja Malezi wa Taasisi ya Ujasiriamali na Ushindani Tanzania (TECC), Bw. Daniel Mghwira (katikati) akizungumza kuhusu kuanza kwa kwa awamu ya tatu ya program Via Jiandalie Ajira kwa halmashauri zote za Dar es Salaam, Mkindani Mtwara, Dodoma na Kibaha Pwani, kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Rais wa Kujitegemea (PTF),Bi. Haigath Kitala na kushoto Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Chemba ya Wafanyabiashara na Kilimo Tanzania(TCCIA),Bi. Magdalene Mkocha.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala Vijana washauriwa kujiunga na awamu ya tatu ya program ya Via Jiandalie Ajira
yaani makala yote Vijana washauriwa kujiunga na awamu ya tatu ya program ya Via Jiandalie Ajira Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Vijana washauriwa kujiunga na awamu ya tatu ya program ya Via Jiandalie Ajira mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/07/vijana-washauriwa-kujiunga-na-awamu-ya.html
0 Response to "Vijana washauriwa kujiunga na awamu ya tatu ya program ya Via Jiandalie Ajira"
Post a Comment