Loading...

Wana CCM wapigana vikumbo Shinyanga

Loading...
Wana CCM wapigana vikumbo Shinyanga - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Wana CCM wapigana vikumbo Shinyanga, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Wana CCM wapigana vikumbo Shinyanga
link : Wana CCM wapigana vikumbo Shinyanga

soma pia


Wana CCM wapigana vikumbo Shinyanga


Suleiman Abeid, Shinyanga

Mkutano wa Chama cha Mapinduzi
WANACHAMA 16 wa jumuiya za CCM mkoani hapa wamejitokeza kuwania uenyekiti wa mkoa ndani ya Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT) na Jumuiya ya Wazazi (WAZAZI).

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa kwa waandishi wa habari jana mjini hapa na makatibu wa jumuiya hizo, uchukuaji na urejeshaji wa fomu kwa ngazi ya wilaya, mkoa na Taifa, ulifungwa rasmi Julai 10 saa 10 jioni.

Katibu wa UVCCM wa Mkoa, Teddy Salum alisema vijana wanane wamejitokeza kugombea nafasi ya uenyekiti mkoa wa jumuiya hiyo na wengine wanane wakiwania ujumbe wa Baraza Kuu Taifa.

Teddy alitaja waliojitokeza kugombea uenyekiti mkoa kuwa ni, Lucas Magadula, Baraka Shemahonge, Jimotoli Maduka, Maduhu Shiwa, Joseph Jilala, Abel Kaholwe, Hassan Ramadhan na Stambuli Mwombeki huku Mwenyekiti anayemaliza muda wake, Reuben Shigela akishindwa kutetea kiti chake kutokana na umri.

Aliwataja waliojitokeza kugombea ujumbe wa Baraza Kuu Taifa kuwa ni Elikana Machanya, Abdul Ngoromole, Joseph Segagi, Robert Masuka, Abdulrahman Nyerere, Janeth Seni, Clement Madinda na Adili Kombolela.

Kwa UWT waliojitokeza kuwania uenyekiti wa mkoa, ni pamoja na Mwenyekiti anayetetea kiti chake, Angela Paulo na Zipora Pangani aliyewahi kuwa Mkuu wa Wilaya.

Katibu wa UWT wa Mkoa, Angela alitaja wagombea wengine kuwa ni Margareth Abwolo,  Jackline Bulay na Christina Kija na waliojitokeza kuwania ujumbe wa Baraza Kuu Taifa la UWT, ni pamoja na Dk Christina Mzava, Joyce Masunga, Mariamu Nyangaka na Ruth Kibela.

Katibu wa WAZAZI Mkoa, Masanja Salu alisema mpaka siku ya mwisho ya urejeshaji wa fomu ni wagombea watatu tu ndio waliorejesha wakiomba kugombea uenyekiti wa mkoa wa Jumuiya hiyo.

Salu aliwataja waliorejesha fomu kuwa ni Perer Sheria, Alhaji Salum Abdalah na Ibrahimu Kani huku Mwenyekiti anayemaliza muda wake, Willy Mzava akitangaza mapema kujitoa.  

 


Hivyo makala Wana CCM wapigana vikumbo Shinyanga

yaani makala yote Wana CCM wapigana vikumbo Shinyanga Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Wana CCM wapigana vikumbo Shinyanga mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/07/wana-ccm-wapigana-vikumbo-shinyanga.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Wana CCM wapigana vikumbo Shinyanga"

Post a Comment

Loading...