Loading...
title : WATANZANIA WAKERWA NA UWANJA WA TAIFA KUTAJWA KUWA NI NAIROBI CITY STADIUM
link : WATANZANIA WAKERWA NA UWANJA WA TAIFA KUTAJWA KUWA NI NAIROBI CITY STADIUM
WATANZANIA WAKERWA NA UWANJA WA TAIFA KUTAJWA KUWA NI NAIROBI CITY STADIUM
Moto unawaka kwenye mitandao ya jamii hususan ya Twitter, Facebook na Instagram baada ya Watanzania wengi kuonesha kukerwa na kitendo cha gazeti la Daily Mail la Uingereza kuutaja Uwanja wa Taifa wa Dar es salaam kuwa ni Nairobi City Stadium wa Kenya wakati timu ya Everton ilipopambana na Gor Mahia na kushinda kwa bao 2-1,
"Hii ni aibu ya mwaka kwa gazeti lenye heshima zake kama Daily Mail kuutaja uwanja wetu kuwa ni wa Kenya, ikidhihirisha dhahiri kwamba mwandishi huyo aidha ni mbumbumbu ama ana ajenda yake iwe ya binafsi ama ya kutumwa" umesema ujumbe mmoja.
Ujumbe mwingine umeenda mbali na kutuhumu kwamba mwandishi huyo ambaye bila shaka ni wa moja ya mashirika ya habari ya kimataifa alifanya hayo hata wakati wachezaji wa Everton walipowasili Dar es salaam na kupkelewa na Waziri Harrison Mwakyembe ambaye walimtaja kuwa ni "Balozi wa Sportpesa" ambao ni wadhamini wa mchezo huo.
"Upuuzi kama huu unaendelea kujirudia na sisi Watanzania tusikae kimya maana hii sio bure kuna mkono wa mtu hapo" umesema ujumbe mwingine.
Ujumbe mwingine umeenda mbali na kushauri wahusika wa masuala ya habari wasilikalie kimya swala hilo na kuwaomba walitake gazeti hilo pamoja na vyombo vingine vilivyotumia taarifa hiyo isiyo sahihi waombe radhi haraka sana ili iwe fundisho.
Hivyo makala WATANZANIA WAKERWA NA UWANJA WA TAIFA KUTAJWA KUWA NI NAIROBI CITY STADIUM
yaani makala yote WATANZANIA WAKERWA NA UWANJA WA TAIFA KUTAJWA KUWA NI NAIROBI CITY STADIUM Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WATANZANIA WAKERWA NA UWANJA WA TAIFA KUTAJWA KUWA NI NAIROBI CITY STADIUM mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/07/watanzania-wakerwa-na-uwanja-wa-taifa.html
0 Response to "WATANZANIA WAKERWA NA UWANJA WA TAIFA KUTAJWA KUWA NI NAIROBI CITY STADIUM"
Post a Comment