Loading...

Waziri Mkuu Majaliwa awahakikishia haya wawekezaji

Loading...
Waziri Mkuu Majaliwa awahakikishia haya wawekezaji - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Waziri Mkuu Majaliwa awahakikishia haya wawekezaji, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Waziri Mkuu Majaliwa awahakikishia haya wawekezaji
link : Waziri Mkuu Majaliwa awahakikishia haya wawekezaji

soma pia


Waziri Mkuu Majaliwa awahakikishia haya wawekezaji

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewahakikishia uwekezaji wenye tija wawekezaji watakaokuja nchini kwa kuwa Tanzania ni nchi yenye amani, utulivu wa kisiasa na uchumi wenye kukua kwa kasi.
Ameyasema hayo leo (Jumapili, Julai 09, 2017) alipomuwakilisha Rais Dkt. John Magufuli katika maadhimisho ya miaka 60 tangu Mtukufu Aga Khan alipochaguliwa kuwa Imamu Mkuu wa madhehebu ya Shia Ismailia duniani.
Waziri Mkuu amesema Serikali inatambua na kuthamini shughuli mbalimbali zinazofanywa na mtandao wa taasisi za Aga Khan zilizopo hapa nchini, hivyo Serikali itaendelea kushirikiana nao.
Ameupongeza mtandao wa taasisi za Aga Khan kwa kumuunga mkono Rais Dkt. Magufuli katika kutoa kipaumbele cha kuwapa fursa watu wenye kipato cha chini kushiriki katika uzalishaji ili waweze kujikwamua kiuchumi.
“Nawahakikishia kwamba uwekezaji wenu hapa nchini utakuwa na baraka  kwa sababu nchi imetulia kisiasa na uchumi wake unakua kwa kasi. Nawaomba muendelee kuwaalika wanajumuia wa  madhehebu ya Shia Ismailia popote walipo duniani waje kuwekeza nchini fursa bado zipo.”
Kwa upande wake Rais wa Jumuiya ya Madhehebu ya Shia Ismailia Tanzania, Bw. Amin Lakhani ameishukuru Serikali kwa ushirikiano inaowapa na kwamba ameahidi kuendelea kushirikiana nayo katika kuboresha sekta mbalimbali nchini.
Amesema mtandao wa maendeleo wa Aga Khan unatoa huduma mbalimbali zikiwemo za afya, elimu, kilimo na kunaendesha miradi katika mabara ya Afrika na Asia kwa kuwapa fursa watu wenye kipato cha chini kushiriki katika uzalishaji ili kujikwamua kiuchumi.
Awali, Mkuu wa wilaya ya Ilala, Bi. Sophia Mjema aliipongeza taasisi hiyo kwa mpango wake wa  upanuzi wa hospitali na kuongeza vituo 35 vya afya kutoka 15 walivyonavyo.


Hivyo makala Waziri Mkuu Majaliwa awahakikishia haya wawekezaji

yaani makala yote Waziri Mkuu Majaliwa awahakikishia haya wawekezaji Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Waziri Mkuu Majaliwa awahakikishia haya wawekezaji mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/07/waziri-mkuu-majaliwa-awahakikishia-haya.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Waziri Mkuu Majaliwa awahakikishia haya wawekezaji"

Post a Comment

Loading...