Loading...

DC Ikungi aipa mbinu NMB jinsi ya kupata wateja wenye uwezo wa chini

Loading...
DC Ikungi aipa mbinu NMB jinsi ya kupata wateja wenye uwezo wa chini - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa DC Ikungi aipa mbinu NMB jinsi ya kupata wateja wenye uwezo wa chini, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : DC Ikungi aipa mbinu NMB jinsi ya kupata wateja wenye uwezo wa chini
link : DC Ikungi aipa mbinu NMB jinsi ya kupata wateja wenye uwezo wa chini

soma pia


DC Ikungi aipa mbinu NMB jinsi ya kupata wateja wenye uwezo wa chini



Mwambawahabari
Mkuu wa wilaya ya Ikungi mkoani Singida, Miraji Mtaturu, ameyashauri mabenki ikiwemo NMB kubuni bidhaa zitakazowanufaisha Watanzania wasio na uwezo (maskini), ili kuondoa dhana inayowabaguzi ya ‘maskini sio rafiki wa taasisi za kifedha’.
 
Mtaturu ametoa wito huo juzi wakati akizungumza kwenye hafla ya ufunguzi rasmi wa tawi la NMB benki Ikungi.
 
Alisema kuendelea kuamini kwamba maskini sio rafiki wa mabenki,kundi hilo la Watanzania litaendelea kudidimia ndani ya lindi la umaskini.
 
“Kaeni muangalie kundi hili la watu maskini litanufaikaje na huduma zinazotolewa na mabenki ikiwemo ninyi NMB. Kundi hili la Watanzania maskini ili liweze kujikomboa kiuchumi, basi mabenki badala ya kutoa mikopo ya fedha taslimu, toeni mikopo ya mizinga ya nyuki, mabwawa ya kufungia samaki au kuku kwa ajili ya kufunga kibiashara,” alishauri Mtaturu.
 
Akisisitiza,mkuu huyo wa wilaya, alisema ili Mtanzania akiwemo maskini aweze kupata maendekeo ya kweli ni lazima ajiongeze kwa kupata mikopo kutoka kwenye taasisi za kifedha.
 
“NMB ninyi mnakwenda vizuri  na mnakwenda na wakati.Mmeendelea kubuni bidhaa/huduma mbalimbali ambazo zimepelekea kuvutia Watanzania zaidi ya milioni mbili kufungua akaunti kwenye matawi yenu nchini kote,” alisema na kuongeza.
 
“Sasa mmebuni akaunti ya FANIKIWA,ambayo inawalenga wajasiriamali wadogo wakiwemo baba/mama lishe na wauza chips, hongereni sana”.
 
Mtaturu alisema sasa umefika wakati wa kuliangalia upya kundi la Watanzania maskini, ili na lenyewe liweze kushiriki kikamilifu kuipeleka Tanzania kwenye uchumi wa kati.
 
Aidha, Mtaturu ametumia fursa hiyo kuwaalika wakazi wa wilaya ya Ikungi wahakikishe wananufaika kikamilifu na huduma mbalimbali zinazotolewa na tawi la NMB Ikungi.
 
“Najua wazi wakazi  wengi wa wilaya  yetu wameshindwa kunufaika na huduma za kibenki  ikiwemo mikopo, kutokana na benki zote kuwa Singida mjini umbali wa kilometa 45. Sasa NMB imesongeza huduma karibu, tuitumie fursa hii kwa kupata mikopo kwa ajili ya kukuza mitaji na kupanua kilimo kikiwemo cha alizeti,” alisema.
 
Katika hatua nyingine, mkuu huyo wa wilaya huyo,ametumia nafasi hiyo kuipongeza na kuishukuru benki ya NMB, kwa msaada wake wa vifaa tiba kwa kituo cha afya Ikungi vyenye thamani ya shilingi milioni tano.
 
“Naagiza vitanda hivi vitatu vya kujifungulia, vifaa vya kujifungulia, vitanda na magodoro mawili ya kupumzikia wagonjwa na mizani mbili, vitunzwe vizuri viweze kutumika kwa kipindi kirefu,” alisema.
 
Awali  meneja NMB kanda ya kati, Straton Chilongola, alisema msaada huo wa vifaa tiba ni mwendelezo wa NMB kuunga mkono serikali ya awamu ya tano katika kuboresha sekta ya afya.
 
Aidha, alisema benki hiyo imeendelea kubuni bidhaa mbalimbali na zenye kuzingatia mahitaji halisi ya soko kwa wakati husika.
 
“Moja ya bidhaa hizo,ni kampeni ya ‘FANIKIWA’ akaunti ambayo ni mahususi kabisa kwa wajasiriamali wadogo wadogo. Wajasiriamali hao ni pamoja na baba/mama lishe, wauza chipis, wenye maduka ya biashara yakiwemo ya nguo,” alifafanua Chilongola.
 
Akifafanua zaidi,alisema akaunti hiyo inampa fursa mteja kupata mkopo wa shilingi laki tano hadi shilingi 30 milioni.
 
Pia meneja huyo,alisema wanayo akaunti nyingine ya ‘Wajibu’ ambayo ni mahususi kwa ajili ya watoto wenye umri wa miaka 0-18.
 
“Kwa upande wa teknolojia,tuna akaunti ya ‘Chap Chap’. Akaunti hii mteja anaweza kufungua akaunti kwa muda mfupi na papo hapo kupata kadi yake ya ATM, na kuanza kufanya miamala wo wote,” alisema Chilongola.
 
Benki ya NMB, ina matawi zaidi ya 200 na mashine za kutolea fedha zaidi ya 700 nchi nzima.Ina wateja zaidi ya milioni mbili jambo linaloifanya kuwa benki pekee nchini yenye hazina ya wateja wengi kuliko benki zingine zilizopo nchini.


Hivyo makala DC Ikungi aipa mbinu NMB jinsi ya kupata wateja wenye uwezo wa chini

yaani makala yote DC Ikungi aipa mbinu NMB jinsi ya kupata wateja wenye uwezo wa chini Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala DC Ikungi aipa mbinu NMB jinsi ya kupata wateja wenye uwezo wa chini mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/08/dc-ikungi-aipa-mbinu-nmb-jinsi-ya.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "DC Ikungi aipa mbinu NMB jinsi ya kupata wateja wenye uwezo wa chini"

Post a Comment

Loading...