Loading...

Halmashauri Zatakiwa Kutumia Mfumo wa PlanRep

Loading...
Halmashauri Zatakiwa Kutumia Mfumo wa PlanRep - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Halmashauri Zatakiwa Kutumia Mfumo wa PlanRep, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Halmashauri Zatakiwa Kutumia Mfumo wa PlanRep
link : Halmashauri Zatakiwa Kutumia Mfumo wa PlanRep

soma pia


Halmashauri Zatakiwa Kutumia Mfumo wa PlanRep

Mwambawahabari
 
PS1B
Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya Bi. Mariam A. Mtunguja akisisitiza jambo mbele ya watumishi wa umma kutoka mikoa ya Songwe, Iringa, Njombe na Mbeya alipokuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa semina ya siku nane juu ya Mfumo mpya wa  kuandaa Mipango na Bajeti za Mamlaka ya Serikali za Mitaa (PlanRep)   jana Jijini Mbeya. Semina hiyo inaendeshwa Kupitia Programu ya Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Watu wa Marekani (USAID). Watumishi kutoka kada za Maafisa Mipango, Makatibu wa Afya, Wahasibu, Maafisa Tehama, Waganga Wakuu katika ngazi za Mikoa na Halmashauri za mikoa hiyo.
Picha na: Frank Shija – MAELEZO
……………………….
Na: Frank Shija – MAELEZO, Mbeya
Halmashauri ambazo azijafikiwa na Program ya Uimarishaji wa Sekta za Umma (PS3) zashauriwa kutenga fedha katika bajeti zao kwa ajili ya kuziwezesha kuingizwa katika mpango huo wenye tija kwa maendeleo ya taifa.

Ushauri huo umetolewa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya Bibi. Mariam A. Mtunguja wakati akifungua semina ya siku nane kuhusu Mfumo mpya wa kuandaa Mipango na Bajeti katika Mamlaka ya Serikali za Mitaa (PlanRep) jana Jijini Mbeya.

“Tumeona namna ambavyo mfumo huu umeleta mabadiliko makubwa katika maeneo ambayo Program hii ya Uboreshaji  wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) inafanya kazi ni vyema sasa mikoa mingine ikaangalia namna kwa kutenga fedha katika bajeti zao ili iweze kuingizwa katika mradi huu muhimu”, alisema Bibi. Mariam.

Aidha Katibu Tawala huyo ameipongeza PS3 kwa kuendesha mafunzo hayo ambayo kwa namna ya kipekee yanashirikisha hata zile Halmashauri ambazo hazipo katika Programu hiyo jambo linaloonyesha dhamira halisi ya kuleta mageuzi katika mifumo ya sekta za umma.

Kwa upande wake Mwakilishi kutoka Programu ya Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma(PS3) Makao Makuu Dkt. Gemini Mtei amesema kutokana na jitihada na uhitaji wa Serikali katika kuboresha mifumo yake wameanzisha mfumo unaorahisisha mawasiliano ya kielekroniki kwa lengo la kuongeza ufanisi na uwajibikaji katika utoaji wa huduma kwa jamii.
Aliongeza kutokana na teknolojia kubadilika Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Watu wa Marekani wanaendesha mafunzo hayo ili kuwajengea uwezo watendaji wake katika kutumia kwa ufasaha Mfumo huu mpya wa kuandaa Mipango na Bajeti.

Naye Mwakilishi kutoka Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Mamlaka ya Serikali za Mitaa (OR – TAMISEMI), Bw. James Mtatifikolo amesema kuwa PlaRep ni mfumo ambao umelenga kuunganisha mifumo yote na kuwa na kanzi data moja kwa sekta zote za umma.

“Tumekuwa na mifumo mingi ambayo kimsingi imekuwa ikisababisha kuwepo kwa taarifa zinazokinzana, hivyo kupitia mfumo huu mpya matatizo yote yametatuliwa  na kuondoa mkanganyiko iliyokuwa ikijitokeza kutokana na kuwepo kwa mifumo tofautitofauti”, aliongeza Bw. Mtatifikolo.

Semina hii ni muendelezo wa mafunzo yaliyoandaliwa na Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na USAID kupitia Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) kwa lengo la kuwajengea uwezo zaidi ya watumiaji 1,500 wa mfumo huu Tanzania nzima ambapo katika awamu ya kwanza yalihusiha mikoa ya Kanda ya ziwa na Kusini yaliyofanyika katika mikoa ya Mwanza na Mtwara, awamu ya pili inahusisha  mikoa ya Nyanda za Juu Kusini, Mashariki na Magharibi katika mikoa ya Mbeya, Morogoro na Kigoma.


Hivyo makala Halmashauri Zatakiwa Kutumia Mfumo wa PlanRep

yaani makala yote Halmashauri Zatakiwa Kutumia Mfumo wa PlanRep Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Halmashauri Zatakiwa Kutumia Mfumo wa PlanRep mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/08/halmashauri-zatakiwa-kutumia-mfumo-wa.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Halmashauri Zatakiwa Kutumia Mfumo wa PlanRep"

Post a Comment

Loading...