Loading...
title : Mkoa wa Kusini Pemba wajipanga kukabiliana na wimbi la madawa ya kulevya
link : Mkoa wa Kusini Pemba wajipanga kukabiliana na wimbi la madawa ya kulevya
Mkoa wa Kusini Pemba wajipanga kukabiliana na wimbi la madawa ya kulevya
Na Salmin Juma, Pemba
Jumla ya watuhumiwa 6 wa madawa ya kulevya mkoa wa kusini Pemba wametiwa hatiani na jeshi la Polisi kwa uuzaji na ungizaji wa dawa hizo.
Akizungumza na redio Istiqama kamanda wa jeshi la Polisi mkoa wa kusini Pemba, Mh, Mohd Sheikhan Mohd amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Tanausu Gomeza Canu raia wa Hispania, Fabrizio Ravalt raia wa Italy, Saburi Ali Hamad mkaazi wa Msingini, Ramadhan Said Mohd mkaazi wa Chachani,Faki Khamis Ali Mkaazi wa Msingini, na Hamad Juma Hamad mkaazi wa Mtoni.
Sheikhan amesema watuhumiwa wote hao walipandishwa mahakamani na hadi kufikia sasa tayari wameshapatiwa hukumu kwa mujibu wa makosa yao.
Kamanda huyo amesema mkoa wake umekuwa na sifa mbovu ya madawa ya kulevya hivyo jeshi la polisi limejipanga kikamilifu kuhakikisha wanawakamata wale wote wanaojihusisha na madawa hayo ambayo yanapelekea kuathiri wimbi kubwa la vijana na kupelekea kupoteza nguvu kazi ya taifa.
Sheikhan ameyataja baadhi ya maeneo ya mkoa wa kusini Pemba ambayo yameathirika zaidi na dawa hizo ni pamoja na Machomane, Michakaini, Ndugu kitu, Msingini ,Miembeni, Muambe, Kengeja na Mkoani na kuwataka masheha na wazee wa vijiji kushirikiana na jeshi la polisi kwa kulipatia taarifa kwani wananchi wakishiriki kikamilifu hakuna kinachoharibika.
Hivyo makala Mkoa wa Kusini Pemba wajipanga kukabiliana na wimbi la madawa ya kulevya
yaani makala yote Mkoa wa Kusini Pemba wajipanga kukabiliana na wimbi la madawa ya kulevya Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Mkoa wa Kusini Pemba wajipanga kukabiliana na wimbi la madawa ya kulevya mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/08/mkoa-wa-kusini-pemba-wajipanga.html
0 Response to "Mkoa wa Kusini Pemba wajipanga kukabiliana na wimbi la madawa ya kulevya"
Post a Comment