Loading...
title : MTUHUMIWA WA UJAMBAZI AFARIKI KWA KUPIGWA RISASI WAKATI AKITOROKA MKOANI SINGIDA.
link : MTUHUMIWA WA UJAMBAZI AFARIKI KWA KUPIGWA RISASI WAKATI AKITOROKA MKOANI SINGIDA.
MTUHUMIWA WA UJAMBAZI AFARIKI KWA KUPIGWA RISASI WAKATI AKITOROKA MKOANI SINGIDA.
Mkazi wa kijiji cha Shiponga – Hanang Mkoani Manyara anayedaiwa kuwa jambazi, Hamisi Athumani (32), amefariki dunia baada ya kupigwa risasi kiunoni na askari polisi wakati akiwa katika harakati ya kutoroka.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani hapa, ACP Debora Magiligimba, amesema tukio hilo limetokea Agosti 25 mwaka huu saa nane mchana, huko katika kijiji cha Mgori tarafa ya Ngimu wilaya ya Singida.
Amefafanua kuwa Hamisi (marehemu) alipigwa risasi na askari polisi wakati akijaribu kuwatoroka mara baada kuonyesha bunduki aina ya rifle yenye namba 7358 na risasi zake tano.
Amesema bunduki hiyo iliyokuwa imekatwa mtutu na risasi zake tano zilikuwa zimefichwa kwenye soksi, vitu hivyo vilikuwa vilihifadhiwa kwenye mfuko wa sandarusi, na kufichwa chini ya jiwe.
ACP Magiligimba amesema Agosti 23 mwaka huu, mtuhumiwa alikamatwa na wananchi wa kijiji cha Ngamu, na kufikishwa katika kituo cha polisi cha kijiji hicho kwa tuhuma ya kujihusisha na matukio ya ujambazi.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida ACP Debora Magiligimba akionyesha bunduki aina ya rifle iliyokuwa ikimilikiwa na mtuhumiwa wa ujambazi Hamisi Athumani (32) mkazi wa Shiponga-Hanang mkoa wa Manyara anayedaiwa kuitumia kwenye matukio ya ujambazi.
Picha/habari na Nathaniel Limu.
Hivyo makala MTUHUMIWA WA UJAMBAZI AFARIKI KWA KUPIGWA RISASI WAKATI AKITOROKA MKOANI SINGIDA.
yaani makala yote MTUHUMIWA WA UJAMBAZI AFARIKI KWA KUPIGWA RISASI WAKATI AKITOROKA MKOANI SINGIDA. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MTUHUMIWA WA UJAMBAZI AFARIKI KWA KUPIGWA RISASI WAKATI AKITOROKA MKOANI SINGIDA. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/08/mtuhumiwa-wa-ujambazi-afariki-kwa.html
0 Response to "MTUHUMIWA WA UJAMBAZI AFARIKI KWA KUPIGWA RISASI WAKATI AKITOROKA MKOANI SINGIDA."
Post a Comment