Loading...
title : NEWS ALERT: SERIKALI KUTANGAZA ZABUNI YA MRADI WA STIEGLER'S GORGE AGOSTI 30, 2017
link : NEWS ALERT: SERIKALI KUTANGAZA ZABUNI YA MRADI WA STIEGLER'S GORGE AGOSTI 30, 2017
NEWS ALERT: SERIKALI KUTANGAZA ZABUNI YA MRADI WA STIEGLER'S GORGE AGOSTI 30, 2017
Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani amesema kuanzia Agosti 30 mwaka huu, Serikali itatangaza zabuni ya kuanza ujenzi wa Mradi Mkubwa wa Umeme wa megawati 2100 katika maporomoko ya maji ya Mto Rufiji mkoani Pwani eneo la Stiegel’s Gorge
Akizungumza jijini Dar es Salaam Dkt. Kalemani amesema, taratibu za awali zimeshaanza ambapo wataalaumu wa ndani na nje wameshakutana na kuchagua sehemu za kujenga mradi huo katika Mto Rufiji, ambapo tayari Shirika la Umeme Nchini ( Tanesco ) limeanza upembuzi yakinifu wa kujenga miundombinu ya umeme na Wakala wa barabara nchini (Tanroad) kujenga miundombinu ya barabara.
Ujenzi wa mradi wa umeme wa megawati 2100 kutoka maporoko ya maji ya Mto Rufiji Mkoani Pwani ( Stiegler’s Gorge)unatarajiwa kuanza ndani ya kipindi cha miezi miwili ijayo baada ya taratibu za zabuni kukamilika, Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani amewambia watanzania kuwa, tayari Serikali imetenga fedha za kutekeleza mradi huo, na hatua za awali za utekelezaji zimekwisha fanyika, ambapo tarehe 30 ya mwezi huu wa Agosti Serikali itatangaza zabuni kwa wakandarasi wa ndani na nje ya nchi ili waweze kuomba kufanya kazi .
Dkt. Kalemani amesema mkandarasi atakayepewa kazi ya kujenga mradi huo ni yule tu atayeridhia kujenga kwa gharama nafuu na kwa muda mfupi zaidi ya uliowekwa Pia Dkt. Kalemani anatoa ufafanuzi namna ambavyo Serikali imejiandaa katika kutekeleza mradi huo.
Kwa mujibu wa Dkt Kalemani, mradi huo utakapokalimilika utakasaidia kuimarisha upatikanaji wa huduma ya umeme nchini na kwamba Serikali haitarajii kuongeza bei ya umeme.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dk. Medard Kalemani akishuka kwenye boti kwa ajili ya kuelekea kwenye eneo la Stieglers Gorge kutakapojengwa mradi huo.
Hivyo makala NEWS ALERT: SERIKALI KUTANGAZA ZABUNI YA MRADI WA STIEGLER'S GORGE AGOSTI 30, 2017
yaani makala yote NEWS ALERT: SERIKALI KUTANGAZA ZABUNI YA MRADI WA STIEGLER'S GORGE AGOSTI 30, 2017 Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala NEWS ALERT: SERIKALI KUTANGAZA ZABUNI YA MRADI WA STIEGLER'S GORGE AGOSTI 30, 2017 mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/08/news-alert-serikali-kutangaza-zabuni-ya.html
0 Response to "NEWS ALERT: SERIKALI KUTANGAZA ZABUNI YA MRADI WA STIEGLER'S GORGE AGOSTI 30, 2017"
Post a Comment