Loading...
title : NIDA YATOA MSAADA WA COMPUTER 200 KWA MKOA WA DAR ES SALAAM,RC MAKONDA NSAEMA ZITAGAWIWA KWA VITUO VYA POLISI 2O,KWAJILI YA KUWEZESHA MFUMO WA KISASA WA KUDHIBITI UHALIFU
link : NIDA YATOA MSAADA WA COMPUTER 200 KWA MKOA WA DAR ES SALAAM,RC MAKONDA NSAEMA ZITAGAWIWA KWA VITUO VYA POLISI 2O,KWAJILI YA KUWEZESHA MFUMO WA KISASA WA KUDHIBITI UHALIFU
NIDA YATOA MSAADA WA COMPUTER 200 KWA MKOA WA DAR ES SALAAM,RC MAKONDA NSAEMA ZITAGAWIWA KWA VITUO VYA POLISI 2O,KWAJILI YA KUWEZESHA MFUMO WA KISASA WA KUDHIBITI UHALIFU
mwambawahabari
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda leo amepokea Jumla ya Computer za kisasa 100 zenye thamani ya Shillingi Million 210 kutoka kiwanda cha utengenezaji wa nguo zitokanazo na pamba ya Tanzania cha NIDA Textile Ltd.
Mhe. Makonda amesema Computer hizo atazitoa kwa Vituo vya Polisi 20 kwaajili ya kufungwa mfumo wa kisasa wa kuripoti taarifa za uhalifu zilizoripotiwa kwenye Vituo vya Polisi kila siku (Crime Statistic Management Information System) kupambana na uhalifu.
Faida za Mfumo ni kumsaidia Mwananchi kupata taarifa za ndugu yake aliepotea pasipokujua yupo wapi kwa kumuangalia kwenye mfumo kama anashikiliwa kwenye Kituo cha Polisi mfumo utaonyesha taarifa zake kwa wakati kwenye kila Kituo.
Aidha mfumo utasaidia viongozi kupata taarifa za uhalifu zinazoripotiwa katika vituo vya Polisi kwa wakati na kupunguza uhalifu kwani taarifa zote za wahalifu zitaonekana kuanzia ngazi ya Mkuu wa Mkoa, Kamanda wa Mkoa,Wilaya na Mkuu wa kituo hivyo kusaidia viongozi kufanya maamuzi.
Mfumo pia utaondoa Rushwa na matukio ya Wananchi kubambikiziwa kesi kwani kila atakaefikishwa kituo cha Polisi viongozi wote akiwemo Mheshiniwa Makonda atapata atajua.
Mfumo pia utamuwezesha kiongozi kujua idadi na aina ya uhalifu unaofanyika kwa siku,eneo ambapo matukio hujirudia mara kwa mara sanjari na mhalifu ambae matukio matukio yake ya uhalifu yamekuwa yakijirudia maeneo mbalimbali.
“Tunaachana na kuandika taarifa kwenye makaratasi na makaunta au madaftari kwenye Vituo vya Polisi ambayo baada ya muda mfupi yanapotea na kumuacha Mwananchi hajui kesi yake imeishia wapi, huu mfumo ni ukombozi na mwonekano mpya wa Jeshi la Polisi na hata Wananchi wataachana na matatizo ya rushwa na watu kubambikiziwa kesi” Alisema Makonda.
Mfumo wa CSMIS utachukuwa taarifa za Mhalifu kuanzia anapoingia kituo cha polisi CRO, Jina la Mhalifu, Aina ya kesi,jina la Mpelelezi, Hakimu, Mahakama anayopelekwa na kama amehukumiwa kulipa faini au kifungo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kiwanda cha NIDA Bwana Mohamed Hamza amesema kampuni yao imeamua kuunga mkono jitiada za Mheshimiwa Makonda katika dhamira yake ya kufanya Mabadiliko ya mfumo wa utendaji kazi wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Dar es Salaam.
Hivyo makala NIDA YATOA MSAADA WA COMPUTER 200 KWA MKOA WA DAR ES SALAAM,RC MAKONDA NSAEMA ZITAGAWIWA KWA VITUO VYA POLISI 2O,KWAJILI YA KUWEZESHA MFUMO WA KISASA WA KUDHIBITI UHALIFU
yaani makala yote NIDA YATOA MSAADA WA COMPUTER 200 KWA MKOA WA DAR ES SALAAM,RC MAKONDA NSAEMA ZITAGAWIWA KWA VITUO VYA POLISI 2O,KWAJILI YA KUWEZESHA MFUMO WA KISASA WA KUDHIBITI UHALIFU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala NIDA YATOA MSAADA WA COMPUTER 200 KWA MKOA WA DAR ES SALAAM,RC MAKONDA NSAEMA ZITAGAWIWA KWA VITUO VYA POLISI 2O,KWAJILI YA KUWEZESHA MFUMO WA KISASA WA KUDHIBITI UHALIFU mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/08/nida-yatoa-msaada-wa-computer-200-kwa.html
0 Response to "NIDA YATOA MSAADA WA COMPUTER 200 KWA MKOA WA DAR ES SALAAM,RC MAKONDA NSAEMA ZITAGAWIWA KWA VITUO VYA POLISI 2O,KWAJILI YA KUWEZESHA MFUMO WA KISASA WA KUDHIBITI UHALIFU"
Post a Comment