Loading...

OPERESHANI MAALUMU YA KUPAMBANA NA KILIMO CHA BANGI, WATANO MBARONI MVOMERO … EKARI 25 ZATEKETEZWA

Loading...
OPERESHANI MAALUMU YA KUPAMBANA NA KILIMO CHA BANGI, WATANO MBARONI MVOMERO … EKARI 25 ZATEKETEZWA - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa OPERESHANI MAALUMU YA KUPAMBANA NA KILIMO CHA BANGI, WATANO MBARONI MVOMERO … EKARI 25 ZATEKETEZWA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : OPERESHANI MAALUMU YA KUPAMBANA NA KILIMO CHA BANGI, WATANO MBARONI MVOMERO … EKARI 25 ZATEKETEZWA
link : OPERESHANI MAALUMU YA KUPAMBANA NA KILIMO CHA BANGI, WATANO MBARONI MVOMERO … EKARI 25 ZATEKETEZWA

soma pia


OPERESHANI MAALUMU YA KUPAMBANA NA KILIMO CHA BANGI, WATANO MBARONI MVOMERO … EKARI 25 ZATEKETEZWA

Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dk Kebwe Stephen Kebwe (aliyeshika dumu) akimimina mafuta ili kuchoma lundo la bangi iliyokuwa imeng’olewa Augosti 19, 2017 na kikosi kazi maalumu katika moja ya mashamba ya bangi katika kitongoji cha Lufuna, Kijiji cha Masalawe, Kata ya Luale , Tarafa ya Mgeta, wilaya ya Mvomero .

Na John Nditi, Globu ya Jamii - Morogoro

POLISI mkoani Morogoro kwa kushirikiana na Maofisa wa Mamlaka ya Kuthibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini wamefanikiwa kuteketeza mashamba ya bangi ya ukubwa wa zaidi ya ekari 25 na kuwatia mbaroni watu watano akiwemo Mwenyekiti wa Kitongoji cha Lufuna , Asteri Telesphor (27). Watu hao miongoni mwao ni Mwenyekiti wa Kitongoji hicho baada ya kukutwa wakijihusisha  na  kilimo  bangi kwa njia ya umwagiliaji kando kando ya mto Mgeta, katika kijiji cha Masalawe, Kata ya Luale , wilayani Mvomero.

Operesheni hiyo maalumu ya kupambana na dawa za kulevya hasa kilimo cha bangi iliyofanyika  Augosti 19, mwaka huu   na kuongozwa Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama  mkoa , Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dk Kebwe Stephen Kebwe akiwa na  Maofisa wa mamlaka ya kuthibiti na kupambana na dawa za kulevya  pamoja na viongozi wa wilaya ya Mvomero.
Viongozi mbalimbali wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama mkoa wa Morogoro na wilaya ya Mvomero walioongozwa na Mkuu wa mkoa Dk Kebwe Stephen Kebwe pamoja na askari Polisi wakiwa katika zoezi la kung’oa na kufyeka miche ya bangi kwenye moja ya mashamba ya bangi katika kitongoji cha Lufuna , Kijiji cha Masalawe, Kata ya Luale , Tarafa ya Mgeta, wilaya ya Mvomero .

Timu ya Opereshani hiyo ililazimika kuacha magari eneo la kijiji cha Homboza , Kata  Mlali  na kutembea kwa miguu kwa  muda wa zaidi  ya saa mbili kufika katika   vitongoji vya Lufuna na Tagata  vilivyopo kijiji cha Masalawe , kata ya Luale , Tarafa ya Mgeta , wilayani Mvomero  kwa ajili ya kutekeleza mashamba hayo. Kugundulika kwa mashamba hayo ni kufuatia   Vyombo vya Ulinzi na Usalama vya mkoa kupata  taarifa kutoka kwa wasiri juu ya uwepo wa uzalishaji mkubwa wa bangi eneo hilo.

Akizubngumza katika eneo la mashamba hayo , Kamishina wa Operesheni wa Mamlaka hiyo, Mihayo Msikhela alisema  , opereshani za kutekeleza dawa za kulevya hasa mashamba ya bangi  ni endelevu  kwenye maeneo mbalimbali nchini na kwa kushirikiana na vyombo vya Ulinzi na Usalama vya mikoa husika .

“ Serikali imekataza matumizi ya dawa za kulevya ikiwemo bangi na ili kutokomeza jambo hii opereshani za kushitumiza zitaendelea kufanyik maeneo mbalimbali nchini na kwamba serikali haijaribiwi” alisema Mihayo.
Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dk Kebwe Stephen Kebwe ( mbele ) akivuka mto Mgeta akifuatiwa na Kamishina wa Operesheni wa Mamlaka ya Kuthibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini, Mihayo Msikhela , Aug 19, 2017 ili kushiriki na kikosi kazi maalumu kwa ajili ya kuteketeza shamba la bangi iliyolimwa kwa njia ya kilimo cha umwagiliaji kando kando mwa mto huo , katika kitongoji cha Lufuna , Kijiji cha Masalawe, Kata ya Luale , Tarafa ya Mgeta, wilaya ya Mvomero .

Naye  Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei alisema ,  watu watano walikamatwa katika opereshani hiyo akiwemo Mwenyekiti wa Kitongoji cha Lufuna , Kijiji cha Masalawe , Kata ya Luale Tarafa ya Mgeta , Asteri Telesphor (27) baada ya kukutwa  na kiroba cha bangi iliyoivuna kutoka shambani mwake.



Hivyo makala OPERESHANI MAALUMU YA KUPAMBANA NA KILIMO CHA BANGI, WATANO MBARONI MVOMERO … EKARI 25 ZATEKETEZWA

yaani makala yote OPERESHANI MAALUMU YA KUPAMBANA NA KILIMO CHA BANGI, WATANO MBARONI MVOMERO … EKARI 25 ZATEKETEZWA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala OPERESHANI MAALUMU YA KUPAMBANA NA KILIMO CHA BANGI, WATANO MBARONI MVOMERO … EKARI 25 ZATEKETEZWA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/08/opereshani-maalumu-ya-kupambana-na.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "OPERESHANI MAALUMU YA KUPAMBANA NA KILIMO CHA BANGI, WATANO MBARONI MVOMERO … EKARI 25 ZATEKETEZWA"

Post a Comment

Loading...