Loading...
title : RC MAKONDA KUTATUA CHANGAMOTO ZA ELIMU.
link : RC MAKONDA KUTATUA CHANGAMOTO ZA ELIMU.
RC MAKONDA KUTATUA CHANGAMOTO ZA ELIMU.
Maria Kaira Mwambawahabari
Mkuu wa mkoa wa Dar es saalam Paul Makonda amedhamiria kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya elimu ikiwemo utatuzi wa majengo 402 ya waalimu pamoja na upungufu wa vyoo katika shule za msingi na sekondari.
Ikiwa changamoto hizo zimekuwa zikiwakabili kwa muda mrefu na imekuwa fedheha kwa waalimu hao katika kuinua maendeleo ya elimu ya mkoa na kumpatia mwanafunzi fursa ya kutimiza ndoto yake ni lazima kutatua changamoto hizo.
Haya yamezungumzwa leo na mkuu wa mkoa wa Dar e s saalam Paul Makonda wakati akizungumza na vyombo vya habari juu ya utatuzi wa changamoto hizi kwa kushirikiana na mainginia kutoka jeshi la wananchi, jeshi la magereza na jeshi la kujenga taifa.
“Ofisi hizo za kisasa zitakuwa na sehemu ya Chumba cha Mwalimu Mkuu,Chumba cha Muhasibu, Chumba cha Katibu pamoja na ofisi ya Mwalimu mkuu msaidizi na walimu wote pamoja na Bafu na Vyoo vya kisasa.Piaujenzi wa ofisi za walimu wa shule ya msingi ni ofisi 295 na shule ya sekondari ni ofisi 107 ndizo zinazotarajiwa kujengwa”amesema
Aidha mh Makonda amewataka wadau mbalimbali wanaopenda sekta ya elimu kusonga mbele kujitokeza kwa wingi kuchangia elimu ya mkoa ili kuweza kutatua changamoto hizi zinazoikabili sekta ya elimu .
Hata hivyo Mheshimiwa Makonda amesema amefanikiwa kupata Mabati 11,000 na mifuko ya Saruji 1,000 ikiwa alikuwa na uhitaji wa Mabati yapatao 50,000, ili kukamilisha ujenzi huo.
Hivyo makala RC MAKONDA KUTATUA CHANGAMOTO ZA ELIMU.
yaani makala yote RC MAKONDA KUTATUA CHANGAMOTO ZA ELIMU. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala RC MAKONDA KUTATUA CHANGAMOTO ZA ELIMU. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/08/rc-makonda-kutatua-changamoto-za-elimu.html
0 Response to "RC MAKONDA KUTATUA CHANGAMOTO ZA ELIMU."
Post a Comment