Loading...

RC SHINYANGA AFANYA MKUTANO WA HADHARA KUSIKILIZA KERO ZA WANANCHI MJINI SHINYANGA

Loading...
RC SHINYANGA AFANYA MKUTANO WA HADHARA KUSIKILIZA KERO ZA WANANCHI MJINI SHINYANGA - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa RC SHINYANGA AFANYA MKUTANO WA HADHARA KUSIKILIZA KERO ZA WANANCHI MJINI SHINYANGA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : RC SHINYANGA AFANYA MKUTANO WA HADHARA KUSIKILIZA KERO ZA WANANCHI MJINI SHINYANGA
link : RC SHINYANGA AFANYA MKUTANO WA HADHARA KUSIKILIZA KERO ZA WANANCHI MJINI SHINYANGA

soma pia


RC SHINYANGA AFANYA MKUTANO WA HADHARA KUSIKILIZA KERO ZA WANANCHI MJINI SHINYANGA

Jumatatu Agosti 21, 2017, Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack (aliyesimama pichani) alifanya mkutano wa hadhara katika viwanja vya Zimamoto karibu na soko la Nguzo Nane Mjini Shinyanga kusikiliza kero za wananchi. 

Mkuu huyo wa mkoa wa Shinyanga aliyekuwa ameambatana na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa,na watumishi mbalimbali wa serikali alisikiliza kisha kujibu kero za wananchi huku pia akitoa nafasi kwa watumishi kutoka idara mbalimbali kujibu hoja na kero za wananchi. 

Miongoni mwa kero zilizoibuka eneo la mkutano huo ni pamoja na ardhi ambapo baadhi ya wananchi walieleza kutoridhishwa namna ardhi inavyotolewa na jinsi migogoro ya ardhi inavyotatuliwa. 

Kero nyingine ni ukosefu wa maadili kwa baadhi ya askari polisi waliodaiwa kutowajali wananchi wanaofika katika kituo cha polisi huku askari polisi wakiendelea kufanya mambo yao ikiwemo kuchat kwenye mitandao ya kijamii badala ya kuhudumia wananchi wanaofika kituoni.
Mkutano unaendelea,viongozi wakiandika dondoo muhimu/maswali ya wananchi

Suala la vumbi katika barabara ambazo ujenzi wake haukamiliki mjini Shinyanga nalo likiibuka kwamba afya zao ziko hatarini kutokana na vumbi hilo. Pia wananchi wakaomba kuwekewa taa za barabarani pamoja na askari wa usalama barabarani katika eneo la Japanese Corner mjini Shinyanga ambapo panadaiwa kutokea ajali za mara kwa mara. 

Kero ya bei kubwa ya maji nayo haikusahaulika,wananchi walieleza kuwa bei ya maji inayotozwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira katika manispaa ya Shinyanga (SHUWASA). Hali kadhalika wananchi wakaomba kuwekewa sehemu ya kupumzikia walau wawekewe mwamvuli katika mahakama ya Mwanzo mjini Shinyanga.
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga,Simon Haule akizungumza

Wananchi pia waliomba kuongezwa kwa waganga katika kituo cha afya Kambarage ambacho kinadaiwa kuzidiwa na idadi ya wagonjwa wanaofika kupata huduma. Wazee nao wakatoa kilio chao cha kutaka huduma bora ya afya wakiomba kuingizwa kwenye bima ya afya badala ya kupewa tu dawa bure. 

Akijibu hoja mbalimbali za wananchi, Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Zainab Telack aliwataka watumishi wa umma kuzingatia maadili yao ya kazi katika kuwatumikia wananchi huku akiwasisitiza kutatua kero za wananchi kwa wakati.
Katibu tawala mkoa wa Shinyanga, Albert Msovela akijibu hoja za wananchi


Telack alitumia fursa hiyo kuwaomba wananchi kutoa taarifa pale inapotokea mkandarasi anayejenga barabara mjini hajamwaga maji kwenye barabara kwani wamemwagiza kuwa anamwaga maji ili kuepusha vumbi. Aidha baada kusikiliza kero za wananchi, mkuu huyo wa mkoa aliagiza kupewa taarifa ya utekelezaji wa mambo mbalimbali waliyokubaliana wakati wa mkutano huowa hadhara ifikapo Septemba 15,2017 ili kuhakikisha kero za wananchi zinapungua. 



Hivyo makala RC SHINYANGA AFANYA MKUTANO WA HADHARA KUSIKILIZA KERO ZA WANANCHI MJINI SHINYANGA

yaani makala yote RC SHINYANGA AFANYA MKUTANO WA HADHARA KUSIKILIZA KERO ZA WANANCHI MJINI SHINYANGA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala RC SHINYANGA AFANYA MKUTANO WA HADHARA KUSIKILIZA KERO ZA WANANCHI MJINI SHINYANGA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/08/rc-shinyanga-afanya-mkutano-wa-hadhara.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "RC SHINYANGA AFANYA MKUTANO WA HADHARA KUSIKILIZA KERO ZA WANANCHI MJINI SHINYANGA"

Post a Comment

Loading...