Loading...
title : SIMIYU KUFANYA MAPINDUZI YA KILIMO KUPITIA UMWAGILIAJI
link : SIMIYU KUFANYA MAPINDUZI YA KILIMO KUPITIA UMWAGILIAJI
SIMIYU KUFANYA MAPINDUZI YA KILIMO KUPITIA UMWAGILIAJI
Na Stella Kalinga, Simiyu.
Mkoa wa Simiyu umejipanga kufanya mapinduzi ya Kilimo kupitia skimu kubwa ya Umwagiliaji inayotarajiwa kuanza kutekelezwa hivi karibuni, kwa lengo la kuwainua wananchi Kiuchumi na kukabiliana na upungufu wa chakula.
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa huo, Mhe.Anthony Mtaka katika kikao kilichofanyika kati ya Viongozi na Wataalam ngazi ya Mkoa,Wilaya na wananchi wa vijiji vya Kata ya Mwamanyili Wilayani Busega kujadili juu ya mipango ya utekelezaji wa skimu hiyo.
Amesema katika Skimu hiyo Halmashauri ya Wilaya ya Busega itaingia mkataba na kukopa fedha kutoka Benki ya Maendeleo ya Kilimo(TADB) ambayo tayari imekubali kutoa mkopo huo, ili kuwezesha ujenzi wa miundombinu ya maji kutoka Ziwa Victoria kwenda kwenye mashamba, kuwawezesha wananchi kununua mbegu bora, mbolea, na zana bora za kilimo.
Aidha, ameeleza kuwa wananchi katika skimu hiyo watazalisha mpunga kwa misimu miwili kwa mwaka na kupanda mazao mengine mbadala hususani ya jamii ya mikunde mara baada ya kuvuna mpunga, kwa ajili ya kurutubisha Ardhi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka akizungumza na wananchi wa Kata ya Mwamanyili, juu ya Skimu ya Umwagiliaji unaotarajiwa kuanza kutekelezwa hivi karibuni katika kata hiyo Wilayani Busega.
Mkuu wa Wilaya ya Busega, Mhe.Tano Mwera akizungumza na wananchi wa Kata ya Mwamanyili, juu ya Skimu ya Umwagiliaji inaotarajiwa kuanza kutekelezwa hivi karibuni katika kata hiyo Wilayani Busega.
Baadhi ya wananchi wa Kata ya Mwamanyili wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka (hayupo pichani) katika kikao cha kujadiliana juu ya Skimu ya Umwagiliaji inayotarajiwa kuanza kutekelezwa hivi karibuni katika kata hiyo Wilayani Busega.
Ndg.Shadrack Yohana Mkazi wa Kijiji cha Nasa Ginnery Kata ya Mwamanyili,akichangia jambo katika kikao cha Viongozi wa Mkoa, Wilaya ya Busega na wananchi kilichofanyika katika Kijiji cha Mwamanyili, kwa lengo la kujadili juu ya Skimu ya Umwagiliaji inayotarajiwa kuanza kutekelezwa hivi karibuni katika kata hiyo Wilayani Busega.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala SIMIYU KUFANYA MAPINDUZI YA KILIMO KUPITIA UMWAGILIAJI
yaani makala yote SIMIYU KUFANYA MAPINDUZI YA KILIMO KUPITIA UMWAGILIAJI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala SIMIYU KUFANYA MAPINDUZI YA KILIMO KUPITIA UMWAGILIAJI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/08/simiyu-kufanya-mapinduzi-ya-kilimo.html
0 Response to "SIMIYU KUFANYA MAPINDUZI YA KILIMO KUPITIA UMWAGILIAJI"
Post a Comment