Loading...

TBS yapewa tuzo na ofisi ya Waziri Mkuu kwa kusaidia wajasiriamali

Loading...
TBS yapewa tuzo na ofisi ya Waziri Mkuu kwa kusaidia wajasiriamali - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa TBS yapewa tuzo na ofisi ya Waziri Mkuu kwa kusaidia wajasiriamali, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : TBS yapewa tuzo na ofisi ya Waziri Mkuu kwa kusaidia wajasiriamali
link : TBS yapewa tuzo na ofisi ya Waziri Mkuu kwa kusaidia wajasiriamali

soma pia


TBS yapewa tuzo na ofisi ya Waziri Mkuu kwa kusaidia wajasiriamali

SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS), limepata tuzo na kushika nafasi ya pili kwa taasisi za kiserikali zinazosaidia wajasiriamali wadogo.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam jana Mkurugenzi Mkuu wa TBS Profesa Egid Mubofu alisema tuzo hiyo intoka Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi kiuchumi (NEEC), katika mwaka wa fedha 2016/2017 TBS na wameshika nafasi ya pili kwa taasisi zinazosaidia wajasiriamali kujimudu kiuchumi.
“Tuzo hii ni chachu kwetu, inatukumbusha kufanya kazi zaidi kwa ajili ya kuiua wajasiriamali wadogo. Hivyo tunawakumbusha wajasiriamali waje kwa wingi nasi tupo tayari kuwasaidia ili azma ya serikali ya viwanda itimie,” alisema Profesa Mubofu na kuongeza:
“Shirika limekuwa likitenga fedha kwa ajili ya kuwahudumia wajasiriamali wadogo, kwa mwaka huu tumetenga kiasi cha Sh milioni 100 kwa ajili hiyo.”
Akizungumzia utaratibu huo unavyofanya kazi Profesa Mubofu alisema: “Tunawasaidia wajasiriamali kupata alama ya ubora bila kulipia gharama yoyote. Utaratibu huu umekuwa ukifanyika kwa kushirikiana na Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO).
“Ambapo mjasiriamali hutakiwa kwenda SIDO kupewa elimu ya msingi ya uzalishaji kisha anatambulishwa kwetu ili tuendeleze elimu na pia kumsaidia katika kuanzisha na kukuza kiwanda. TBS tunamgharamia mjasiriamali huyo kila kitu kuanzia ukaguzi hadi kumpatia leseni ya kutumia alama ya ubora.”
Aidha, wajasiriamali wadogo wanafanikiwa kupata leseni ya kutumia alama ya ubora kupitia mpango huu huendelea kuhudumiwa bure  na shirika kwa kipindi cha miaka mitatu: “kuanzia mwaka wan ne watatakiwa kuchangia asilimia 25 ya malipo, mwaka wa tano asilimia 50 na mwaka wa sita asilimia 75 hadi ikifika mwaka wa saba watatakiwa kulipia asilimia 100 ili kupata fursa ya kusaidia wajasiriamali wanaochipukia.”
Vilevile ili kuimarisha na kurahisisha utendaji kazi katika mkakati huu, TBS na SIDO wanatarajia kusaini hati ya makubaliano ili kurahisisha utendaji kazi wa kuwahudumia wajasiriamali.
TBS kwa muda mrefu sasa wamekuwa wakishirikiana na taasisi na mamlaka nyinyine za kiserikali  kuhakikisha wajasiriamali wadogo wanaanzisha viwanda vidogo kabisa, vidogo na vya kati ili kutimiza azma ya Serikali ya Awamu ya Tano kuwa ifikapo mwaka 2025 Tanzania iwe na uchumi wa kati utokanao na viwanda.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango nchini (TBS), Prof. Egid Mubofu akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari kufuatia kupata tuzo iliyotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia Baraza la Uwezeshaji wananchi Kiuchumi (NEEC) kutokana na mchango wa Taasisi hiyo katika kuchangia maendeleo na uakuaji wa wajasiriamali nchini jijini Dar es Salaam.


Hivyo makala TBS yapewa tuzo na ofisi ya Waziri Mkuu kwa kusaidia wajasiriamali

yaani makala yote TBS yapewa tuzo na ofisi ya Waziri Mkuu kwa kusaidia wajasiriamali Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala TBS yapewa tuzo na ofisi ya Waziri Mkuu kwa kusaidia wajasiriamali mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/08/tbs-yapewa-tuzo-na-ofisi-ya-waziri-mkuu.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "TBS yapewa tuzo na ofisi ya Waziri Mkuu kwa kusaidia wajasiriamali"

Post a Comment

Loading...