Loading...

Uchumi wa Tanzania Waendelea Kuimarika-Dkt. Abbasi

Loading...
Uchumi wa Tanzania Waendelea Kuimarika-Dkt. Abbasi - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Uchumi wa Tanzania Waendelea Kuimarika-Dkt. Abbasi, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Uchumi wa Tanzania Waendelea Kuimarika-Dkt. Abbasi
link : Uchumi wa Tanzania Waendelea Kuimarika-Dkt. Abbasi

soma pia


Uchumi wa Tanzania Waendelea Kuimarika-Dkt. Abbasi


By Bushiri Matenda-MAELEZO

Licha ya kuyumba kwa uchumi na kuongezeka kwa mfumuko wa bei duniani, Tanzania imeendelea kuongoza kwa ukuaji wa uchumi miongoni mwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki ambapo takwimu za Benki Kuu ya Tanzania (BOT) na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) zimetaja uchumi wa Tanzania kuwa imara.

Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi alibainisha hayo wakati akitoa ufafanuzi kwa Waandishi wa Habari leo Jijini Dar es Salaam kuhusu hali ya uchumi nchini.

“Uchumi wa Tanzania kwa miaka mitatu mfululizo sasa bado uko katika ukuaji usiopungua asilimia 7.0 hadi 7.2 ikiwa ni ukuaji wa juu katika ukanda wa Afrika Mashariki ambapo Rwanda inakua kwa asilimia 6, Uganda asilimia 5 na Kenya asilimia 6.4”, alisema Dkt. Abbasi.

Alieleza kuwa sambamba na ukuaji wa uchumi, Tanzania imeendelea kudhibiti mfumuko wa bei ambapo taarifa ya hivi karibuni zilizotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) zinaonesha kuwa mfumuko wa bei nchini umeshuka kutoka asilimia 6.1 mwezi Mei hadi kufikia asilimia 5.4 mwezi Juni mwaka huu.

Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Hassan Abbasi akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hali ya uchumi nchini leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara hiyo Sehemu ya Habari na Picha Bw. Rodney Thadeus.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Hassan Abbasi (hayupo pichani) alipokuwa akiwasilisha mada kuhusu hali ya uchumi mbele ya waandishi wa habari leo Jijiji Dar es Salaam.
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mkurugenzi Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Hassan Abbasi akiwasilisha mada kuhusu hali ya uchumi wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam.
Picha zote na: MAELEZO.




Hivyo makala Uchumi wa Tanzania Waendelea Kuimarika-Dkt. Abbasi

yaani makala yote Uchumi wa Tanzania Waendelea Kuimarika-Dkt. Abbasi Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Uchumi wa Tanzania Waendelea Kuimarika-Dkt. Abbasi mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/08/uchumi-wa-tanzania-waendelea-kuimarika.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Uchumi wa Tanzania Waendelea Kuimarika-Dkt. Abbasi"

Post a Comment

Loading...