Loading...

UTAFITI WA KUGEMA UTOMVU WA KUTENGENEZEA BAZOKA (CHEWING GUM) PAMOJA NA GEL WAANZA KATIKA SHAMBA LA MITI LA SAO HILL

Loading...
UTAFITI WA KUGEMA UTOMVU WA KUTENGENEZEA BAZOKA (CHEWING GUM) PAMOJA NA GEL WAANZA KATIKA SHAMBA LA MITI LA SAO HILL - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa UTAFITI WA KUGEMA UTOMVU WA KUTENGENEZEA BAZOKA (CHEWING GUM) PAMOJA NA GEL WAANZA KATIKA SHAMBA LA MITI LA SAO HILL, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : UTAFITI WA KUGEMA UTOMVU WA KUTENGENEZEA BAZOKA (CHEWING GUM) PAMOJA NA GEL WAANZA KATIKA SHAMBA LA MITI LA SAO HILL
link : UTAFITI WA KUGEMA UTOMVU WA KUTENGENEZEA BAZOKA (CHEWING GUM) PAMOJA NA GEL WAANZA KATIKA SHAMBA LA MITI LA SAO HILL

soma pia


UTAFITI WA KUGEMA UTOMVU WA KUTENGENEZEA BAZOKA (CHEWING GUM) PAMOJA NA GEL WAANZA KATIKA SHAMBA LA MITI LA SAO HILL


Shamba la miti la Sao Hill likishirikiana na Kampuni ya Art International limeanza utafiti wa kugema utomvu wa miti ya msindano kama njia ya kujiongezea kipato.

Akizungumza na Kamati ya Bunge ya Maliasili na Mabadiliko ya tabia ya nchi ya nchini Malawi iliyotembelea Shamba la Miti la Sao Hill, Meneja wa Shamba hilo Salehe Beleko amesema katika kuongeza vyanzo vya mapato wameingia mkataba na kampuni hiyo kufanya utafiti na ikibainika kwamba haitaathiri ukuaji wala ubora wa miti wataidhinisha kuwa chanzo kipya cha mapato.

Akifafanua Salehe Baleko amesema wanatarajia kuuza kila kilo moja ya utomvu kwas h. 750. Beleko amesema kwa kuwa ni utafiti wameanza kwanza na miti iliyokuwa tayari kuvunwa wakiona hakuna madhara wataendelea kwenye miti michache yenye umri mdogo na matokeo ya utafiti huo yatapelekea ama kukuza ama kukataza kabisa zoezi hilo.

Naye mtaalamu wa kampuni ya uchina, Yhoung Zhoung amesema taasisi yake imefuata taratibu zote za ugemaji na usafirishaji wa utomvu huo na amefafanua kwamba kampuni yake inahitaji miti millioni mbili kwa mwaka ilikupata ujazo wa utomvu wanauhitaji

Akijibu swali la mke wa Rais wa zamani wa Malawi, Patricia Muluzi ambaye pia ni mjumbe wa kamati hiyo ambaye alitaka kujua matumizi ya utomvu huo mtaalamu huyo amesema baada ya kuchakatwa na kuchanganywa na kemikali mbalimbali utomvu huo hutumika kutengenezea dawa mbalimbali bazoka (chewing gum) pamoja na gel

Mjumbe wa Kmaati hiyo, Rashid Pemba Msusa, amesema kwa mara ya kwanza wameshuhudia matumizi mapya kabisa ya zao la mti teknolojia ambayo hawajawahi kuiona nchini kwao Malawi. Hata hivyo ameahidi kufuatilia matokeo ya utafiti huo ili ukifaa wauhamishie Malawi.
Mti aina ya msindano ambao umegemwa utomvu katika Shamba la miti la Sao Hill lililoko Mufindi mkoani Iringa ikiwa ni utafiti unaofanywa na Kampuni ya Art International kwa kushirikiana na shamba hilo ikiwa ni njia ya kujiongezea kipato.
Meneja wa Shamba la miti la Sao Hill, Salehe Baleko akikinga utomvu unaotoka katika mti wa msindano ambao baada ya kugemwa huchakatwa na kuchanganywa na kemikali mbalimbali ambao hutumika kutengenezea dawa mbalimbali ikiwemo bazoka (chewing gum) pamoja na gel. (Picha na Wizara ya Maliasili na Utalii) 
Mtaalamu wa Kampuni ya Art International, Zhoung Yhoung akitoa maelezo kuhusu zoezi la ugemaji wa utomvu kwa ujumla unaofanywa na kampuni yake (Picha na Wizara ya Maliasili na Utalii) 


Hivyo makala UTAFITI WA KUGEMA UTOMVU WA KUTENGENEZEA BAZOKA (CHEWING GUM) PAMOJA NA GEL WAANZA KATIKA SHAMBA LA MITI LA SAO HILL

yaani makala yote UTAFITI WA KUGEMA UTOMVU WA KUTENGENEZEA BAZOKA (CHEWING GUM) PAMOJA NA GEL WAANZA KATIKA SHAMBA LA MITI LA SAO HILL Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala UTAFITI WA KUGEMA UTOMVU WA KUTENGENEZEA BAZOKA (CHEWING GUM) PAMOJA NA GEL WAANZA KATIKA SHAMBA LA MITI LA SAO HILL mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/08/utafiti-wa-kugema-utomvu-wa.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "UTAFITI WA KUGEMA UTOMVU WA KUTENGENEZEA BAZOKA (CHEWING GUM) PAMOJA NA GEL WAANZA KATIKA SHAMBA LA MITI LA SAO HILL"

Post a Comment

Loading...