Loading...
title : Vijana Zaidi ya 60 Wamlalamikia Muwekezaji Kwa Kukosa Malipo Yao.
link : Vijana Zaidi ya 60 Wamlalamikia Muwekezaji Kwa Kukosa Malipo Yao.
Vijana Zaidi ya 60 Wamlalamikia Muwekezaji Kwa Kukosa Malipo Yao.
Kinamama wa kijiji cha Sambaru wakiendelea kutwanga mawe kwa ajili ya kuweka tayari kwa kupatikana madini ya ya zahabu
baadhi ya vijana wa kijiji cha sambaru
Na Woinde Shizza,Singida
Zaidi ya vijana 60 wa kijiji cha Sambaru kata ya Ikungi wilayani Igungi mkoani Singinda wamemlalamikia mwekezaji wa kampuni ya Sambaru Gold Mining kwa kitendo cha kuwarusha fedha za malipo ya kazi walikuwa wakimfanyia mgodini kwake
Wakiongea na waandishi wa habari kijijini hapo baadhi ya vijana hao walisema kuwa wamefanya kazi katika kampuni hiyo kwa kipindi cha mda mrefu lakini muwekezaji huyo ajawalipa ela zao na badala yake amewafukuza kazini hapo bila kuwalipa malipo yoyote .
Mmoja wa vijana hao aliyejitambulisha kwa jina la Saidi Hassan alisema kuwa walishapeleka malalamiko yao kwa viongozi wa kijiji lakini hakuna hatua yeyote iliyochukuliwa hivyo wameiomba serikali iwasaidie ili wapate mafao yao kwani fedha hizo walikuwa wanazitegemea katika kuwasaidia katika majukumu mbalimbali ya kifamilia.
“tumekuwa tunamfata muwekezaji huyu na kumuomba atulipe fedha zetu lakini amekuwa anatukana na kusema atudai ,mbaya zaidi kunawakati alifikia hatua ya kukamata baadhi ya wenzetu ambao wanamdai na kuwapeleka polisi,”alisema Saidi
Kwa upande wake kijana mungine aliyejitambulisha kwa jina la Fredy John alisema kuwa kunakipindi walishawahi kumpeleka polisi alipofika na kuulizwa kama vijana hao wanamdai alikuabali na akahaidi kuwalipa na aliomba mda na akapewa kimaandishi lakini ,muda huo umepita na hadi leo vijana hao awajalipwa na amefikia hatua ya kuwakana kabisa
Gazeti hili lilimtafuta mwenyekiti wa kijiji hicho cha Sambaru Mfaume Hassan ili kubainisha kama anataarifa za vijana hawa nae alisema kuwa ni kweli anataarifa za vijana hawa na alishamtumia mmiliki wa kampuni hiyo taarifa za kuwalipa vijana hawa lakini hajateleza hivyo ameamua kupeleka swala hili katika ngazi za juu ili wamsaidie
“sisi kama kijiji tumekuwa tuna utaratibu wa kuwapa vijana wawekezaji hawa nah ii inatokana na uhitaji wa muwekezaji ,unakuta muwekezaji anataka vijana wa kumsaidia kazi uko mgodini kwake analeta barua katika ofisi ya kijiji na sisi tunampa vijana na ndio utaratibu uliofanywa sasa muwekezaji huyu kaja kuchukuwa vijana lakini cha kushangaza wamefanya kazi mgodini kwake lakini ajawalipa mpaka leo na mbaya zaidi akifatwa anasema kuwa adaiwi kitu ambacho sio cha kweli mimi kama kiongozi wa kijiji nikishirikiana na wenzangu tutajitaidi kufuata sheria ili vijana hawa walipwe ela zao na hadi sasa navyoongea nilishampa taarifa mkuu wa wilaya”alisem Mwenyekiti wa kijiji Mfaume Hassan
Gazeti hili lilimtafuta mmiliki wa kampuni ya Sambaru Gold Mining Ahamed Magoma kujibu tuhuma hizi nae alisema kuwa yeye kama yeye adaiwi na kijana yeyote Yule wa kijiji cha Sambaru ,na kama kuna mtu anae mdai afuate vyombo husika vya sheria akamdai
“mimi sidaiwi na kijana yeyote Yule vijana wangu wote ambao nawaajiri nawalipa vizuri na wengine wapo kazini hadi sasa,pia mimi sijawai kwenda kijijini kutafuta kijana wa kunifanyia kazi na napenda kusema ivi kama kuna mtu ambae ananidai afuate sheria ,aje na vielelezo anidai na kama ni kweli nitamlipa ila sidaiwi na mtu yeyote “alisema Magoma
Akiongelea swala hilo mkuu wa wilaya ya Ikungi Miraji Mtaturu alisema kuwa swala hilo alishalipokea kutoka kwa mwenyekiti wa kijiji cha Sambaru na alimuagiza aandike idadi ya vijana hao pamoja na majina yao ili ayafanyie kazi ,aidha pia alisema kuwa atamuandikia barua ya kumuita ofisini kwake mmiliki wa mgodi huo wa Sambaru Gold Mining .
Hivyo makala Vijana Zaidi ya 60 Wamlalamikia Muwekezaji Kwa Kukosa Malipo Yao.
yaani makala yote Vijana Zaidi ya 60 Wamlalamikia Muwekezaji Kwa Kukosa Malipo Yao. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Vijana Zaidi ya 60 Wamlalamikia Muwekezaji Kwa Kukosa Malipo Yao. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/08/vijana-zaidi-ya-60-wamlalamikia.html
0 Response to "Vijana Zaidi ya 60 Wamlalamikia Muwekezaji Kwa Kukosa Malipo Yao."
Post a Comment