Loading...
title : Wakili: Sethi kupoteza maisha asipotibiwa haraka
link : Wakili: Sethi kupoteza maisha asipotibiwa haraka
Wakili: Sethi kupoteza maisha asipotibiwa haraka
Makandege alidai hayo jana mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi na kueleza mahakama kuwa mshitakiwa huyo alifanyiwa upasuaji na kuwekwa puto tumboni.
Alidai kuwa katika mashauri yaliyopita, mahakama ilitoa amri mara mbili, zote zikielekeza mshitakiwa huyo apelekwe Hospitali ya Muhimbili lakini haijatekelezwa.
Aliomba mahakama izingatie ugonjwa wa mshitakiwa na iamuru apelekwe moja kwa moja Muhimbili kwani ndio hospitali ya juu ya serikali nchini ambayo inategemea kuwa na wataalamu na vifaa stahiki vya ugonjwa unaomkabili.
"Upande wa jamhuri unatambua haya lakini kwa ridhaa yao wao wamempeleka mshitakiwa Amana hospitali. Swali ambalo mahakama isaidie kujibu pamoja na jamhuri, ni je, kumpeleka mshitakiwa wa kwanza hospitali ya Amana, magereza na jamhuri wameshindwa kutii amri ya mahakama?," alihoji Makandege.
“Mahakama haikumungunya maneno katika kutoa amri yake, ambapo ilitamka kwenye amri hiyo kwamba mshitakiwa huyo apelekwe katika hosipitali ya taifa ya Muhimbili, wao kumpeleka Amana wametekeleza amri gani?” Makandege aliendelea kueleza.
Alidai amri ya mahakama haijatekelezwa hivyo upande wa mashitaka umekaidi amri hiyo."Mahakama ndio mahala amri zote zitaheshimiwa kwa pande zote mbili kwa kuwa nchi inafuata demokrasia na utawala wa sheria," alidai Makandege.
Makandege alidai kuwa kilichofanyika ni kinyume na amri ya mahakama na kinyume na sheria za magereza kifungu cha 53 (1) ambacho kinatoa fursa kwa mtu yoyote aliyeko gerezani kama anaumwa kufikishwa hospital ili apate matibabu.
Hivyo makala Wakili: Sethi kupoteza maisha asipotibiwa haraka
yaani makala yote Wakili: Sethi kupoteza maisha asipotibiwa haraka Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Wakili: Sethi kupoteza maisha asipotibiwa haraka mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/08/wakili-sethi-kupoteza-maisha.html
0 Response to "Wakili: Sethi kupoteza maisha asipotibiwa haraka"
Post a Comment